Katika msafara wa utekelezaji kwa raia (Alwafaa lilmuwatwin) unaofadhiliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na kutekelezwa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, umewasili katika mkoa wa Mosul ukiwa na zaidi ya shehena mia mbili za misaada mbalimbali, kwa watu wa kabila la Aizidiyyiin wanaoishi katika miji wa Sanjaar, Ba’ashiqa na Bahzani.
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi kutoka mikoa kumi na mbili wameshiriki katika msafara huu pamoja na ofisi mbalimbali za Alwafaa, hawajaishia kutoa msaada wa vitu peke yake, bali wamekutana na viongozi mbalimbali wa Aizidiyyiin na wakristo pamoja na kutembelea makanisa, wamekutana na wafungwa wa kikristo kwa ajili ya kuimarisha uhusiano wa raia wa Iraq na kuonyesha mshikamano pamoja na waathirika wa ugaidi katika miji hiyo.
Kumbuka kua msafara huu nisehemu ya misafara mingi iliyo fanywa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, ambapo walitembelea vituo vya Hashdi Sha’abi na maeneo mengine, pia siku za nyuma wamesha wahi kuwatembelea Aizidiyyiin na kuonyesha kushikamana nao kutokana na machungu waliyo pitia ya kunyanyaswa na kuteswa na magaidi wa Daesh.