Kazi ya uwekaji wa vizuwizi imeanza ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kutenganisha wanaume na wanawake

Maoni katika picha
Miradi ya ujenzi inaendelea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambapo mradi wa mwisho ulikua uwekaji wa marumaru, na kuweka mazingira mazuri ya urembo yanayo endana na maeneo mengine ya jengo, kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kazi ya kuweka vizuwizi vyenye urefu maalum na uimara mkubwa vikizungukwa na tabaka la vioo na nakshi za mapambo yanayo endana na haram kwa ajili ya kutenganisha upande wa wanaume na wanawake, kazi hii imesanifiwa na kutekelezwa na kitengo hicho bila msaada wa watu wa nje, vizuwizi hivyo vimechukua nafasi ya vizuwizi vya zamani vilivyo wekwa kwa muda ambavyo vilikua vinaanguka kutokana na kusukumwa na mazuwaru hasa wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi hii ni sehemu ya kazi nyingi zinazo fanywa na wataalamu wa kitengo cha mafundi na wahandisi, zinazo lenga kuiweka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika muonekano mzuri, na kumuwezesha zaairu mtukufu aweze kufanya ibada kwa amani na utulivu, kazi ya uwekaji wa vizuwizi hivyo ni sehemu ya miradi mingi tunayo ifanya, hii ni kwa sababu vizuwizi vya kwanza vilivyo kua vimetengenezwa kwa vyuma na kuvishwa mbao vilikua vimeisha, ndipo tukabuni vizuwizi hivi ambavyo ni imara zaidi na vinavyo tarajiwa kua vya kudum”.

Akaongeza kua: “Vizuwizi hivi ni vizuri na imara, vinaweza kuvumilia harakati za mazuwaru, vimewekwa vizuri na vinaendana na vigingi vitakavyo wekwa pande mbili, upande wa kicha kitukufu wenye urefu wa mita (14) na vitakua na kimo cha mita mbili, na upande wa miguuni wenye urefu wa mita (13) na kimo kile kile (mita mbili), vimetengenezwa kwa vifaa imara pamoja na vioo vya max na inatabaka tatu kila moja inaunene wa (sm 8).

Akabainisha kua: “Kuhusu nakshi na mapambo yaliyo wekwa yanaendana na mapambo yaliyopo katika haram tukufu, fahamu kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya kina nafasi kubwa ya kubuni na kujenga sehemu nyingi za Atabatu Abbasiyya tukufu, sehemu ya ndani na nje ya Ataba, inamafundi na wataalamu waliobobea katika fani mbalimbali”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: