Idara ya mahusiano ya vyuo inaendelea na ratiba ya (Mjadala wa kitamaduni)

Maoni katika picha
Mwaka wa pili mfululizo idara ya mahusiano na vyuo vikuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa harakati za mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, inaendelea na rakiba ya kiutamaduni (Mjadala wa kitamaduni), ambao ni kusambaza mabango yaliyo andikwa hadithi za Mtume (s.a.w.w) pamoja na hadithi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s), zenye mafundisho ya malezi na akhlaq na zinazo himiza elimu na kusoma na maadili mema, sambamba na kufundisha uzalendo wa taifa.

Ratiba hii ni sehemu ya mradi mkubwa unaolenga kuwajenga wanafunzi katika imadi ya Dini, sambamba na kuinua kiwango cha ubora wa elimu ambacho kwa sasa kinaendelea kushuka, mradi huu umeratibiwa vizuri na wataalamu wa idara ya elimu na unawahusu wavulana na wasichana, kwa kufuata umri wao na uwezo wa uwelewa wao.

Idara za shule, vyuo na maahadi zimepongeza hatua hii iliyo chukuliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na umuhimu wake kwa wanafunzi, kwani njia zote zinazo tumika kuwafundisha na kuwaelezea ni nzuri, zinawafanya wapate elimu sahihi kwa njia sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: