Kitengo cha Dini charatibu mihadhara kuhusu bibi Fatuma Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Hakika miongoni mwa jambo gumu zaidi ni kuelezea utukufu wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) na baba yake Mtume (s.a.w.w), ni sawa na kusema kua: yupo juu ya uwezo wa kalamu, ulimi, maelezo na ubainifu, kwa ajili ya kuchota jopo kidogo katika bahari mkubwa usiokauka, kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya kimeratibu utowaji wa mihadhara ya Dini kuhusu hadithi tukufu (…juu ya kueleweka kwake katika karne za kwanza), siku mbili kwa wiki kwa ajili ya kutoa fursa kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mazuwaru ya kuweza kuhudhuria.

Kuhusu ratiba hiyo, Shekh Ali Mohani kutoka kitengo cha Dini amesema kua: “Mihadhara hiyo inalenga kuelezea utukufu wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), ukizingatia kua yeye anahadhi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hii ni ratiba moja miongoni mwa ratiba nyingi zinazo pangwa na kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanyika kama hivi katika matukio mengi ya kumbukumbu za kuzaliwa au kufariki kwa mmoja wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.

Akaendelea kusema: “Tumechagua mihadhara hii izungumzie siri za bibi Fatuma Zaharaa (a.s), tunajaribu kuzama katika bahari yake na kuchota mazuri yake, kisha kuyazungumza katika mihadhara hatua kwa hatua, kila muhadhara utasherehesha hadithi tukufu: (… juu ya kueleweka kwake katika karne za mwanzo), na ilikua vipi Manabii na Mitume (a.s) waliamrisha umma zao zimtambue Swidiiqatu Kubra (a.s) na wote walitambua utukufu wa bibi huyu (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: