Kuanza sehemu ya tano ya mradi wa kuweka marumaru kwenye jengo la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kazi ya kuweka marumaru katika jengo la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inaendelea na inaonekana wazi, sehemu zinazo jengwa zimeanza kukamilika moja baada ya nyingine, kazi imefika hatua ya tano katika eneo la katikati ya milango miwili, mlango wa Imamu Mussa bun Jafari (a.s) na mlango wa Imamu Hassan (a.s) upande wa magharibi ya haram tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh: “Uwekaji wa marumaru za chini na katika kuta za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umekamilika kwa kiasi kikubwa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu utakamilika ndani ya muda uliopangwa”.

Akaendelea kusema: “Watendaji wa mradi huu wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanamaliza kazi walizo pewa, wataalamu wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya wananafasi kubwa katika utendaji wa kazi kwani wanashirikiana nasisi bega kwa bega, wao ndio waliofanya kazi za awali katika mradi huu”.

Akabainisha kua: “Kazi za awali zilihusisha mambo mengi kabla ya kuingia rasmi katika mradi, miongoni mwa kazi hizo ni; kukata sehemu zilizo kua na madini kwa ajili ya kuwapa nafasi mafundi ya kuondoa marumaru za zamani, kurepea ukuta wa chini na kuziba mipasuko, kuweka tabaka la chuma ambalo juu yake zinawekwa marumaru sambamba na kutandika mfumo wa umeme na mawasiliano”.

Kumbuka kua marumaru mpya zimetengenezwa kwa kufuata vipimo maalumu vinavyo endana na sehemu zinapo wekwa sawa iwe ni ukutani au chini, zimekaguliwa mara nyingi na kuthibiti uimara wake pamoja na uhalisi wa rangi zake, pamoja na mambo mengine mengi ambayo yamefanya marumaru hizi kuwa bora zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: