Kitengo cha malezi na elimu ya juu chawapa mafunzo ya mambo ya habari watumishi wake

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinawapa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wake, kila mmoja anapewa mafunzo kutokana na sekta yake, ikiwa ni pamoja na mafunzo ya sekta ya habari, wameratibu mafunzo ya sekta ya habari yanayo endana na maendeleo yaliyopo katika sekta hiyo.

Mafunzo hayo yatachukua siku (14) kila siku watakaa darasani kwa muda wa saa mbili, mafunzo haya yanaendeshwa kwa kushirikiana na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kilicho andaa wakufunzi wenye uweledi mkubwa katika sekta hii.

Ustadh Ali Khabbaaz ambaye ni kiongozi wa idara ya habari katika kitengo cha habari na utamaduni cha Ataba, naye ni mmoja wa wakufunzi katika mafunzo haya, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mada ya leo imekamilisha mada zilizo tolewa kabla ya leo kwa mujibu wa ratiba, imefafanua kwa kina njia za kuandika na kuchambua kilicho andikwa kwa kufuata kanuni zake, kama vile kanuni ya mfunguo, mchokozo, mzunguko na kanuni ya mtangulizo”.

Akabainisha: “Mada zijazo zitahusu mambo yanayo husiana na kuhariri habari kwa kutumia njia ya maandishi na fani zake mbalimbali, kama inavyo toa fursa kubwa kwa mtangazaji, sambamba na kuangalia vyombo vya habari vya kielektronik na namna ya kujiepusha na matumizi mabaya na kuhakikisha vinatumika vizuri”.

Kumbuka kua semina hii imehusisha watumishi wa sekta ya habari walioajiriwa katika shule za Al-Ameed, wanajengewa uwezo ili kuongeza ufanisi katika kazi zao na waweze kuripoti mambo kwa uhalisia wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: