Kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat cha Atabatu Abbasiyya tukufu cha chukua jukumu la kufundisha mada mbili kwa wanafunzi wa kitengo cha elimu za maktaba katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya

Maoni katika picha
Katika kuendeleza ushirikiano na kufanyia kazi makubaliano yaliyopo baina yao, kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat chini ya maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mwaka wa pili mfululizo kimekua kikifundisha mada mbili kwa wanafunzi wa hatua ya kwanza na ya pili wa kitengo cha elimu za maktaba wa kitivo cha adabu katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya, kituo kimechukua jukumu hili baada ya kupokea ombi rasmi kutoka kwa mkuu wa kitivo hicho, kutokana na uzowefu walio nao wataalamu wake katika maswala ya maktaba na kuwafanya kuwa na uwezo mkubwa wa kufunzisha mambo ya kisekula.

Ustadh Ahmadi Muhammad Abdul-Amiir mmoja wa wakufunzi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat cha maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya kimechukua jukumu la kufundisha njia za kisasa zaidi za utaratibu wa faharasi unaotumika duniani kwa sasa, kwa wanafunzi wa hatua ya kwanza (RDA) na kanuni ya (MARC21) tunafundisha somo la faharasi kwa kufuata kanuni zake, katika hatua ya kwanza tunafundisha faharasi za vitabu na ujumbe mkuu, katika hatua ya pili tunafundisha aina za faharasi”.

Akaongeza kua: “Kila wiku kunakua na mihadhara miwili kwa kila hatua, muhadhara wa kwanza unakua wa nadhariya kuhusu maktaba, kisha maktaba itafundisha mada mbili za ziada, na mada ya pili ya vitendo, kanuni hizo zitafanyiwa kazi katika muhula ujao wa masomo”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu ametuwezesha kufikisha elimu kwa wanafunzi na kupata mafanikio makubwa katika mwaka uliopita, tunatarajia mwaka huu utakua sawa na mwaka jana, wanafunzi wanamwitikio mkubwa sana”.

Kumbuka kua maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu inamkataba wa ushirikiano na chuo kikuu cha Mustanswiriyya, katika uendeshaji wa makongamano, warsha na utowaji wa mafunzo katika mambo mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: