Kwa ajili ya kuongeza uzuri katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s): imeanza kazi ya kuweka mapambo katika madirisha

Maoni katika picha
Wataalamu wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya wameanza kazi ya kuweka mapambo katika madirisha ya haram tukufum ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ili madirisha hayo yachukue nafasi ya madirisha ya zamani yaliyo wekwa miaka mingi iliyo pita, pamoja na kuongeza uzuri na kupendezesha muonekano wake, na kuifanya iwe na mandhari zuri zaidi kwa mazuwaru watukufu.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Hassan Mussa ametuambia kuhusu kazi hii kua: “Hii ni sehemu ya kazi zinazo fanywa na wataalamu wa kitengo chetu katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), nayo ni sehemu ya kukamilisha miradi iliyo kamilika, kama vile mradi wa kuweka kashi karbalai katika jengo, huku madirisha yakiendelea kubaki kama yalivyo kua, sasa ni wakati wa kubadirisha madirisha na kuweka mapya yatakayo ongeza uzuri wa jengo, madirisha yametengenezwa na mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kua: “Yametengenezwa kwa mbao bara zaidi, baada ya kuchukua vipimo maalumu kwa kila dirisha, madirisha mapya yametengenezwa kwa mbao na yamewekwa mapambo kwa ndani, yameandikwa (Yaa qamaru bani Hashim), yamezungushiwa uduara wenye upana ya (sm 10) na unene wa (sm 7), yamefunikwa na mapambo yanayopitisha hewa”.

Kumbuka kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitendo muhimu, kina idara nyindi na mafundi pamoja na wahandisi wa fani mbalimbali, kinafanya kazi usiku na mchana katika vitengo vyote vya Ataba tukufu kwa ajili ya kuhakikisha Ataba inatoa huduma bora kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: