Juhudi kubwa inafanywa na wataalamu wa idara ya ufundi ya kitengo cha eneo tukufu la katikati ya haram mbili

Maoni katika picha
Wengi wao ni wanajeshi wasio julikana miongoni mwa watumishi wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wanafanya juhudi kubwa katika kutekeleza majukumu yao, watu hao ni wataalamu wa idara ya ufundi katika kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili ambacho kipo chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kama alivyo tuambia kiongozi wa idara hiyo Ustadh Fadhili Hussein idara hiyo imefanya kazi nyingi katika eneo hilo la kijografia, pamoja na eneo la barabara ya Maitham Tammaar hadi barabara ya Shuhadaa, sambamba na eneo la katikati ya haram mbili na maeneo yanayo zunguka sehemu hiyo.

Idara ya ufundi ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili kama alivyo bainisha Husseiniy: “Majukumu yake yamegawanyika sehemu nyingi, miongoni mwa sehemu hizo ni: ufundi chuma, ufundi rangi, umwagiliaji pamoja na ukarabati na mapambo”. Akaongeza kua: “chuma hutumika kutengeneza mabanda, ngazi na vizuwizi sehemu za ukaguzi, nguzo za feni, nguzo za kamera na kutengeneza mitambo inayo tumiwa na kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu pamoja na nguzo za umeme”.

Kuhusu kazi za kupaka randi akasema: “Upakaji wa rangi huhusisha kupaka rangi katika vifaa vya umeme vilivyopo kwenye eneo la katikati ya haram mbili tukufu na katika barabara kuu zinazo elekea eneo hilo, kuna sehemu nyingi ambazo huhitaji kupakwa rangi katika maeneo ambayo yapo chini ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu”.

Miongoni mwa kazi muhimu zaidi zinazo fanywa na idara ya ufundi ni kazi ya maji, kwa mujibu wa maelezo ya Husseiniy: “kuna feni zinazo nyunyiza maji, kuna mahodhi na mabomba katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kuna mtambo maalum wa maji ya eneo hilo tukufu, pamoja na kuwepo kwa mtandao maalum kwa ajili ya idara ya bustani chini ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu”.

Husseiniy akasema kua: “Kazi za idara hii haziishii katika mambo hayo peke yake, kuna kazi zingine za ufundi kuhusu paa lililopo katika baadhi ya sehemu za eneo la katikati wa haram mbili, husafishwa, hufanyiwa marekebisho na hubadilishwa, pia kuna sehemu ambazo huwekwa zege na njia zingine ambazo zipo ndani ya usimamizi wetu hufanyiwa matengenezo maalumu kwa kuweka smenti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: