Mradi wa vikao vya mazungumzo katika vyuo vikuu: vijana wanauliza maswali kwa ajili ya kutambua haki

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inalipa umuhimu mkubwa swala la elimu katika vyuo vikuu, imesha andaa miradi mingi kwa ajili ya swala hilo, inayo lenga wakufunzi na wanafunzi wa vyuo vikuu, mradi wa vikao vya mazungumzo ni miongoni mwa miradi hiyo, unalenga kuwajenga wanafunzi katika akhlaq, dini na idikadi, na kuwafanya waweze kukabili changamoto za mmomonyoko wa maadili na vita ya kiutamaduni.

Kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya tablighi kimechukua jukumu hili na kuandaa ratiba na mpangilio maalum.

Mkuu wa program hiyo Sayyid Muhammad Mussawiy ambaye ni kiongozi wa idara ya tablighi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ametuambia kuhusu ratiba hii kua: “Wanafunzi wanapewa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani wanafunzi wanachangamoto nyingi, makundi mbalimbali hutaka kuwaharibu na kuwafanya wasitekeleze majukumu yao, kwa ajili ya kupambana na swala hilo; kitengo cha dini kupitia idara ya tabligh kinaendesha program mbalimbali katika vyuo vikuu vya Iraq, miongoni mwa program hizo ni hii ya vikao vya mazungumzo katika vyuo vikuu”.

Akaongeza kua: “Huteuliwa mmoja wa wasomi wa hauza miongoni mwa masayyid na mashekh wa kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuzungumza katika vikao vivyo kisha wanafunzi hupewa nafasi ya kuuliza maswali na yeye kuyajibu, kabla ya kwenda huwa tunafanya mawasiliano na uongozi wa chuo kikuu kwa ajili ya kuchagua kitivo kitakacho kua mwenyezi wa kikao hicho”.

Kuhusu uendeshwaji wa vikao hivyo amesema kua: “Vikao hivyo huwa na mijadala ya wazi, kila mmoja hupewa nafasi ya kueleza mtazamo wake, kwa ajili ya kuangalia uwezo wa wanafunzi katika kujenga hoja sambamba na kuangalia mchango wao katika kujenga jamii, zaidi huangalia upande wa tabia na maadili”.

Kuhusu mfumo wa kikao amesema kua:

  • 1- Maneno elekezi kuhusu mada ya siku hiyo.
  • 2- Kugawa karatasi kwa wanafunzi ili waandike maswali bila kuandika majina yao kisha hukusanywa na kukabidhiwa shekh mtoa mada.
  • 3- Mtoa mada hujibu maswali kwa sauti na kwa uwazi ili wote wapate faida.
  • 4- Majibu yanatakiwa yafungamane na dalili za kielimu, aya za Qur’ani na hadithi za mtume, atumie lugha fasaha inayo eleweka kwa urahisi na wanafunzi waliombele yake sambamba na kuweka vionjo katika majibu yake”.

Akamaliza kwa kusema: “Lengo kubwa la kufanya vikao hivi ni kuimarisha kiwango cha elimu kwa wanafunzi, tunatarajia kuona matokeo chanya katika familia zao na jamii, tuna mshukuru Mwenyezi Mungu tumepata mwitikio mkubwa na usikivu mzuri kwa wanafunzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: