Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kupitia mradi wa Qur’ani wa wanafunzi wa vyuo vikuu uitwao (Ufumbuzi wa matatizo ya wanafunzi kijamii katika Qur’ani), imeandaa nadwa inayofanyiwa katika kitivo cha kilimo kwenye chuo kikuu cha Karbala na kuhudhuriwa na wanafunzi wengi pamoja na walimu wao.
Mtoa mada katika nadwa hiyo ni shekh Haarith Daahi kutoka kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, amezungumzia Qur’ani tukufu na uwelewa wa jamii katika kutatua matatizo ya kijamii kwa kufanya tadabur (mazingatio) katika aya za Qur’ani, na akatafsiri baadhi ya aya zinazo elezea matatizo ya kijamii, akafafanua kua: “Lazima kuwe na uhusiano wa kweli pamoja na Mwenyezi Mungu mtukufu kupitia Qur’ani, uhusiano huo ndio chakula cha roho, lazima kijana mwelewa awe na utamaduni wa kufungamana na Qur’ani pamoja na Husseiniyya, tukitaka kulinda utambulisho wetu lazima tushikamane na kitabu kitukufu pamoja na kizazi kitakasifu”.
Kisha akajibu maswali na mapendekezo kutoka kwa wanafunzi na walimu walio hudhuria.
Kumbuka kua mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu unafanywa kwa mwaka wa sita mfululizo, mwaka jana wanafunzi walio nufaika na mradi huu uliohusisha semina, nadwa, mihadhara, makongamano na mashindano ya Qur’ani walikua zaidi ya (2000), chini ya ratiba maalumu iliyo pangwa, na kuwasiliana na wakuu wa vyuo pamoja na wakuu wa vitivo (michepuo) ili kuepusha kugongana kwa ratiba, pia vimeongezwa vipengele vingine vinavyo endana na uwezo wa akili za vijana hao pamoja na mahitaji yao ya chuoni na nyumbani.