Kwa ajili ya kuweka mazingira ya usalama kwa mazuwaru: Atabatu Abbasiyya tukufu yafunga zaidi ya kamera (800) za ulinzi

Maoni katika picha
Tangu idara ya kisheria ilipo chukua jukumu la kuisimamia Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya mambo mengi, imepiga hatua kubwa katika kuimarisha ulinzi na usalama kutokana na umuhimu wa jambo hilo kwa mazuwaru, ili kuwawezesha kufanya ziara kwa amani na utulivu pamoja na ukosefu wa amani uliolikumba taifa, juhudi kubwa zinafanywa na watumishi pamoja na kufunga mitambo ya kisasa zikiwemo kamera za ulinzi zaidi ya (800) za kisasa zaidi, ambazo zinatumika kwa mara ya kwanza hapa Iraq, kamera hizo zimefungwa zaidi ya sehemu sitini, ndani na nje ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mtandao wa Alkafeel umeingia katika chumba cha kusimamia kamera za ulinzi na kuwakuta wafanyakazi wake wanachapa kazi kama nyuki, wanaangalia kila kitu kidogo na kikubwa kupitia kompyuta na screem, tumefanya mazungumzo na idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo inasimamia mfumo huu muhimu, kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Farasi Abbasi ametuambia kua: “Mfumo wa kamera za ulinzi ulio anzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kabla ya miaka miwili ni mfumo wa kisasa zaidi hapa Iraq, unasifa nyingi zinazo endana na watalamu wa idara hiyo, wana uwezo mkubwa na uzowefu wa kuendesha mfumo huo na kuendelea kuuboresha, mfumo huu ambao ni moja ya mifumo mingi iliyopo unafanya kazi sambamba na mingine, lengo kuu ni kuimarisha amani na utulivu kwa mazuwaru watukufu, na kumkamata kila atakayetaka kuvunja amani, mfumo huu umekua msaada mkubwa kwa vikosi vya ulinzi na usalama vya Ataba tukufu katika kuimarisha ulinzi”.

Akaongeza kua: “Ulinzi umeimarishwa saa (24) kupitia zaidi ya kamera (800) za ulinzi, zimefungwa katika maeneo yafuatayo:

  • - Ndani ya haram takatifu.
  • - Ndani ya ukumbi wa haram tukufu.
  • - Ndani ya sardabu ya haram tukufu na sehemu zilizo ongezwa.
  • - Maeneo yanayo zunguka ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Njia kubwa na ndogo zinazo elekea katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Vituo vya ugaguzi.

Mhandisi Farasi akabainisha kua: “Kupitia mfumo huu wa kamera, tumefanikiwa kudhibiti matukio mengi ya uharifu, wizi na mengineyo, yaliyokua yameanza kuenea kidogo kidogo, tunashirikiana na Atabatu Husseiniyya tukufu pamoja na ofisi ya polisi ya Karbala, hususan katika kuwabaini watu wanao tafutwa kwa mujibu wa sheria, tumefanikiwa kukamata wahalifu wengi kutokana na mafunzo ya usalama waliyo pewa wataalamu wanao simamia mfumo huu”.

Akamaliza kwa kusema: “Tuna mpango wa kupanua eneo la usalama sambamba na kuendelea kumiliki teknolojia ya kisasa zaidi katika mfumo wa kamera za ulinzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: