Tangu idara ya kisheria kuchukua jukumu la kusimamia Atabatu Abbasiyya tukufu, viongozi wakuu walianza kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na utoaji wa huduma pamoja na miradi ya kielimu, kiutamaduni na mingineyo, miradi ya ujenzi imepiga hatua kubwa, ujenzi wa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayo zunguka haram na miradi ya nje.
Mtandao wa kimataifa Alkafeel; ukizingatia kua ndio mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ndio dirisha linaloitangaza, haukua mbali na mafanikio hayo, kutokana na umuhimu wa jambo hili imeandaa ukurasa maalum unao onyesha miradi iliyotekelezwa ndani ya muda wa zaidi ya miaka kumi na tano.
Kila mtu anajua miradi iliyo tekelezwa na inayo endelea kutekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, inayo husu ukumbi wa haram tukufu, kuanzia ukarabati na uwekaji wa marumaru, pamoja na miradi mingine ya sekta ya viwanda, kilimo, tiba, elimu na nyumba za makazi, imetekeleza miradi mingi mizuri ya kupigiwa mfano.
Kwa ajili ya kumrahisishia kila mtu aweze kuona mafanikio hayo, idara ya Intanet chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ndio mwendeshaji wa mtandao wa kimataifa Alkafeel imeandaa ukurasa maalum kwa ajili ya kuonyesha miradi hiyo, ukurasa huo unaitwa: Miradi ya Atabatu Abbasiyya (https://alkafeel.net/projects).
Ukurasa huo unamiradi muhimu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kiwango cha ukamilifu katika miradi hiyo na mahala ilipo pamoja na huduma zinazo tolewa, kila mradi utakao anzishwa utaingizwa katika ukurasa huu pamoja na taarifa zake muhimu, kwa ajili ya kumpa nafasi kila mtu aweze kutambua kazi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu sambamba na kutambua mafanikio yaliyo fikiwa katika sekta ya ujenzi na utowaji wa huduma.