Kituo cha kuongeza elimu na kukuza vipaji Alkafeel chashiriki katika warsha ya program za kompyuta

Maoni katika picha
Kutokana na kuwepo kwa program mpya, kituo cha elimu na kukuza vipaji Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeshiriki katika warsha ya kielimu iliyo andaliwa na kitengo cha program za kompyuta katika maahadi ya ufundi Karbala, warsha ambayo inawashiriki wengi na taasisi zinazo shughulika na sekta hii.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kituo Ustadh Saamir Swafi: “Wameshiriki baada ya kupata mwaliko rasmi kutoka Maahadi ya Karbala, tumeshiriki kwa ajili ya kuongeza elimu na maarifa na kutambulisha program mpya zilizo tengenezwa na kituo, sambamba na kuangalia mfumo (selebasi) ya kufundishia, na uwezekano wa kuitumia pamoja na manufaa yake kielimu, bila kutegemea program zinazo tumiwa na watu wengine, pamoja na kufikisha ujumbe kua akili za watalamu wa Iraq zinaweza kugundua na kutengeneza program mpya za kompyuta”.

Akaongeza kua: “Kituo kilipata nafasi ya kutoa mada iliyo wasilishwa na Mhandisi Mustwafa Tamimiy mmoja wa watumishi wa kituo, alizungumzia mtazamo wa kituo katika utoaji wa program zinazo changia maendeleo ya wanafunzi na kuwatoa katika mfumo wa nadhariya hadi mfumo wa vitendo, miongoni mwa program hizo ni program ya shule “Siraaju” imeonyesha mafanikio makubwa katika shule zinazo itumia, pamoja na mambo mengine ya kitekniko yaliyo zungumzwa katika warsha hiyo”.

Rais wa kitengo cha tekniko na program za kompyuta katika Maahadi ya Karbala Ustadh Waathiq Lufta Abdu-Ali amesema kua: “Hakika hii ni fursa nzuri sana kwetu kukutana na taasisi hizi pamoja na watu wenye elimu na utaalam mkubwa, warsha imejikita katika kuzungumzia program zilizopo katika matumizi hivi sasa pamoja na uwezekano wa kubadilisha selibasi ya wanafunzi wa Maahadi ili iendane na program zilizopo sokoni kwa sasa”.

Mwalimu msaidizi katika kitivo cha uhandisi cha chuo kikuu cha Karbala Dokta Ali Fauzi amesema kua: “Katika warsha hii tumeangalia mahitaji ya soko katika sekta ya program za kompyuta, na tumetoa mihadhara ya maelekezo kwa wanafunzi na wataalamu, ambayo tumeelezea vipengele muhimu vinavyo weza kumsaidia mwanafunzi kupata kazi baada ya kuhitimu masomo yake”.

Mwisho wa warsha; mwakilishi wa kituo alitangaza nafasi za kujiunga na masomo kwa wanao taka kujiendeleza, na akawaambia kua milango ipo wazi kwa ajili yao na watafundishwa kulingana na viwango vyao vya elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: