Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa zawadi kwa zaidi ya wanafunzi elfu moja kwenye hafla ya mwaka wa tano ya wanafunzi wakike wanaovaa Abaa la kiiraq

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya asubuhi ya Ijumaa ya leo (21 Rabiu Thani 1440h) sawa na (28 Desemba 2018m) kimefanya mahafali ya wanafunzi wa kike wanaovaa Abaa ya kiiraq ndani ya uwanja wa chuo, mahafali hii husimamiwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya mahusiano na vyuo katika mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo, hafla imepata mahudhurio makubwa yakiongozwa na mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) pamoja na idadi kubwa ya viongozi, katika mahafali haya zaidi ya wanafunzi elfu moja wamepewa zawadi kutoka chuo kikuu cha Baabil na Al-Ameed pamoja na kutoka katika Maahadi ya ufundi iliyopo katika wilaya ya Musayyabu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo fuatiwa na kisomo cha surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa (Lahnul Ibaa), baada ya hapo ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Kisha ukafuata ujumbe kutoka vyuo vikuu vilivyo shiriki, ulio wasilishwa na mwakilishi wa chuo kikuu cha Baabil Dokta Naajih Ma’amuriy, ambae alisema kua: “Ni utukufu mkubwa kukutana katika uwanja huu mtakatifu ndani ya siku tukufu na kazi tukufu, tumekutana kufanya jambo linalo pendwa na Mwenyezi Mungu na mtume wake na linatukuzwa na sheria pamoja na urfu (mazowea)”.

Akaongeza kua: “Hakika kuhuisha Abaa (vazi) la Zainabiyya katika chuo kinacho toa mafunzo mbalimbali ni jambo zuri, miradi kama hii kusimamiwa na Ataba ni jambo linalo stahili pongezi na shukrani nyingi, japokua sio jambo geni kwa Ataba zetu tukufu”.

Akaendelea kusema: “Jambo hili lilianza kufanywa katika chuo kikuu cha Baabil zaidi ya miaka saba iliyo pita, idadi ya wanafunzi wa kike walioshiriki wakati huo walikua (57) walizawadiwa na wasimamizi wa kongamano la Zaharaa la wanawake, idadi iliendelea kuongezeka kila mwaka pamoja na kuhitimu masomo idadi kubwa ya wanafunzi hao, hadi leo tumefikia idadi hii”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunaushukuru mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo ambao umekua pamoja nasi kwa utukufu wa Alkafeel, pia ni fahari kwetu kuwa pamoja nao, tunaishukuru kamati ya kusapoti Abaa Zainabiyya katika chuo kikuu cha Baabil pamoja na taasisi zote za kimalezi zinazo shiriki katika mradi huu”.

Ukafuata ujumbe wa wanafunzi washiriki ulio wasilishwa na Nuru Jafari, ambae alisema kua: “Mwanamke anatakiwa ainamishe macho yake ili aweze kuhifadhi kilicho amrishwa na Mwenyezi Mungu kuhifadhiwa, pia lazima afuate kanuni zilizo wekwa na Mwenyezi Mungu kwa kutii amri na kutekeleza usia, asionyeshe mapambo yake ispokua kwa wale waliotajwa na Mwenyezi Mungu katika Qur’ani tukufu, na ashushe ushungi wake shingoni na kifuani kwake, lazima atambue kua anatakiwa ajisitiri daima, anatakiwa awe karibu na soksi pamoja na nguo za stara”.

Akaongeza kua: “Mwanamke akishikamana na maelekezo haya, anatakiwa awe msaada muhimu kwa ndugu yake mwanaume, ashirikiane nae katika hafla za kielimu, jihadi, malezi na kulingania dini tukufu, hijabu hamzuii kufanya mambo hayo na wala sio kikwazo”

Hafla ilipambwa na mashairi pamoja na kaswida iliyo somwa na ustadh Ahmadi Zaamiliy, iliyo muelezea bibi Zaharaa (a.s), likafuata shairi lililosomwa na mtoto Muhammad Dhiyaau aliyetaja maneno yaliyo amsha hisia za damu ya mashahidi wa Iraq walio uwawa kwa ajili ya kulinda taifa hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: