Mafundi na wahandisi wa idara ya umeme chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, wamepiga hatua kubwa katika kuweka mtandao wa umeme ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kazi hiyo imehusisha kuanzishwa mfumo maalumu wa umeme wa minara na kuingizwa katika matumizi, kazi hii imekamilika baada ya kufanywa juhudi kubwa na ndani ya muda mfupi.
Kiongozi wa idara ya umeme katika kitengo tajwa Mhandisi Ali Abdulhussein ameongea kuhusu mradi huu kua: “Tulianza kutengeneza mtandao wa umeme ndani ya ghorofa unaopita chuni ya ardhi kuanzia hatua ya kwanza, kuanzia hatua ya kuweka bomba za kupitishia nyaya za umeme wa njia kuu, kisha tukawenya nyaya za umeme wa taa na matumizi mengine”.
Akaongeza kua: “Kebo kuu inawaya wenye ukubwa wa (milimita 25) ambao umetoka katika chumba kikuu cha mitambo ya umeme kilichopo katika sardabu kwa ajili ya kusambaza umeme sehemu mbalimbali wenye ukubwa wa (LED), Usambazaji wa umeme huo umehusisha pia minara, mwanga wake ni mara tatu zaidi ya mwanga uliokuwepo na kwa kiwango kidogo sana cha matumizi ya umeme, tupo katika hatua za mwisho za kufunga taa ndani ya sardabu”.
Akafafanua kua: “Tumefunga njia maalum ya umeme wa dharura katika kila sardabu, pamoja na kufunga taa nyekundu na za kijani katika kaburi, tuko tayali kubadilisha kitakacho hitaji kubadilishwa siku za mbele au kuongeza kitakacho hitajika, pamoja na mahitaji mengine ya umeme yanayo endana na jengo tukufu la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akamaliza kwa kusema: “Kuhusu vituo vya huduma vilivyopo ndani ya haram tukufu, tumeanza kutengeneza njia yake maalum ya ziada, ambayo imepangiliwa kwa ustadi mkubwa kiasi ambacho umeme hauwezi kukatika sehemu hizo tena kutoka kiwango cha (LED) hadi kiwango cha chini kabisa cha matumizi ya umeme, sambamba na sehemu za kutunzia nyama na mitambo mingine mbalimbali inayo hitaji umeme”.
Tunapenda kusema kua; kitengo cha usimamizi wa kihandisi ni moja ya vitengo muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu chenye idara nyingi zinazo husika na mambo mbalimbali, kina mchango mkubwa katika kufanikisha miradi mingi inayo fanywa ndani na nje ya Ataba tukufu.