Maahadi ya Qur’ani imeandaa nadwa kuhusu ufasaha wa Qur’ani

Maoni katika picha
Miongoni mwa mtiririko wa nadwa za kielimu zenye umuhimu mkubwa, Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya imeratibu nadwa ambayo imepewa jina la (ufasaha katika Qur’ani), katika nadwa hiyo amealikwa Ustadh Aqiil Jaburiy kua mzungumzaji, na imepata mahudhurio makubwa ya wapenzi wa kitabu kitukufu pamoja na kundi kubwa la wanafunzi na walimu wa hauza pamoja na waumini.

Jaburiy ameongelea ufasaha (balagha) na umuhimu wake ndani ya Qur’ani, na namna Mwenyezi Mungu alivyo onyesha ufasaha wake mbele ya binaadamu na majini, nayo (Qur’ani) ndio hoja ya Mwenyezi Mungu kwa watu wote na hasa kwa waarabu; kwa sababu imeshushwa kwa lugha ya kiarabu na inaubainifu wa kila kitu, Qur’ani ni hazina ya hekima, elimu na maarifa Mwenyezi Mungu hajaacha chochote, bado kila siku yanaendelea kuonekana maajabu yake na kutoa elimu mpya, ni maneno bora zaidi ya wanayo zungumza waarabu, Jaburiy alizungumzia aya tukufu iliyopo katika surat Huud, kupitia aya hiyo akafafanua makumi ya fani za balagha, ibdaai na fasaha, na akataja mapokeo mengi yaliyo zingumzwa na wanachuoni wakubwa kuhusu ufasaha wa aya hizo.

Kiongozi wa tawi la Maahadi katika mji wa Hindiyya Sayyid Haamid Mar’abiy amebainisha kua: “Hii ni moja ya nadwa endelevu zinazo fanyika kila mwezi, ambazo huandaliwa na tawi la Maahadi na kuwaalika wasomi wa Qur’ani kutoka katika hauza na shule za kisekula, lengo kubwa ni kujaribu kuzama katika hazina za kitabu cha Mwenyezi Mungu katika mada tofauti na kuzizungumza kiutafiti na kwa njia nyepesi inayo eleweka, kwa kiasi ambacho inasaidia kupanua wigo wa kufuata utamaduni wa Qur’ani, hakika nadwa zote hupata mahudhurio makubwa kutoka kwa waumini, wasomi wa kisekula, wanafunzi wa hauza na wadau wa Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: