Idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) imetangaza kufanikiwa kwa safari waliyo kwenda kuwasaidia watu wa kabila la Aizidiy huko Mosul, iliyo pewa jina la: (Ubinaadamu umetuunganisha) amboyo imeshiriki mikoa kumi na mbili na kufanikiwa kufikia lengo.
Kongamano limefanyika ndani ya jengo la Alqamiy makao makuu ya uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, chini ya usimamizi wa kiongozi Shekh Abbasi Akaishi, kilihusisha viongozi wa ustawi wa jamii kutoka katika mikoa iliyo shiriki, Shekh Akaishi alisifu kazi nzuri iliyofanywa na watendaji wa mradi wa safari za (Ubinaadamu umetuunganisha) ya kuwasaidia watu wa kabila la Aizidy katika mji wa Mosul, wakazungumzia mambo muhimu yanayo fanywa na ofisi za idara hiyo, na wakatoa wito wa kusaidia mikoa iliyopata mashahidi wengi katika vita yetu tukufu pamoja na kuweka mpango kazi wa kipindi kijacho.
Shekh Maitham Zaidiy mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji amepongeza juhudi kubwa zilizo fanywa na viongozi wa ofisi za ustawi wa jamii, na mafanikio makubwa yaliyo patikana katika safari ya kuwasaidia watu wa kabila la Aizidiy, msafara huo unatokana na agizo la kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i).
Kumbuka kua msafara wa (Ubinaadamu umetuunganisha) zimeshiriki ofisi za ustawi wa jamii kutoka mikoa kumi na mbili pamoja na msafara wa Alwafaa unaofanywa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, hawakuishia kutoa pesa na chakula peke yake, bali walikutana na wafungwa wakristo kwa ajili ya kuimarisha uhusiano kati ya tabaka mbalimbali za Iraq, kumbuka kua misaada na safari hizo ni sehemu tu ya safari na misaada mingi inayo tolewa na idara ya ustawi wa jamii katika mikoa tofauti, wakati huohuo ukatolewa wito wa kuwasaidia ndugu zetu Aizidiy kutokana na mateso waliyo pata kutoka kwa magaid wa Daesh.