Kuta za vizuwizi vya kuongoza matembezi ya mazuwaru zinaendana na jengo la kaburi tukufu

Maoni katika picha
Kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa juu, mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu wamemaliza kazi ya kuweka ukuta (vizuwizi) vinavyo tenganisha kati ya wanaume na wanawake ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuta hizo zimejengwa kisasa na kwa ustadi wa hali ya juu kwa namna ambayo zinaendana na mapambo yaliyopo katika dirisha tukufu, pia zinaendana na nakshi na mapambo yaliyo wekwa.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu ameelezea sifa za kuta hizo zinazo anzia upande wa kichwa kitakatifu kwenda upande wa miguu, akasema: “Mafundi wetu walianza kutengeneza ukuta wa kutenganisha upande wa wanaume na wanawake, ulio buniwa na kusanifiwa pamoja na kujengwa na wairaq wenyewe bila kutengemea fundi yeyote wa nje, kuta hizo zinasifa zifuatazo:

  • 1- Kuta hizo zimetengenezwa kwa Satanles Steel.
  • 2- Kila kipande ndani yake kina sehemu nyingi na kinatenganishwa na nguzo ya Stanles Steel.
  • 3- Nguzo inayo tenganisha imesimikwa katika ardhi kwa njia maalumu na kwa viwango maalumu.
  • 4- Katikati ya nguzo na nguzo kuna vioo vya Maqsi vyenye tabaka tatu, kila tabaka inaujazo wa milimita (8).
  • 5- Kila kipande kimewekwa nakshi zinazo fanana na zile zilizopo katika dirisha tukufu.
  • 6- Kila nguzo imenakshiwa na neno (Ewe Abbasi) lililo rudiwa rudiwa mawa (12).
  • 7- Sehemu ya kioo inamzunguko uliotengenezwa na Stanles Steel kwa ajili ya uimara zaidi.
  • 8- Kimo cha ukuta ni mita mbili (2).
  • 9- Kuta hizo zimewekwa pande mbili, upande wa kichwa kitukufu, wenye urefu wa mita (14), na upande wa miguu wenye urefu wa mita (13)”.

Kumbuka kua kazi hii ni sehemu ya kukamilisha miradi inayo fanywa ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambayo mradi wake wa mwisho ulikua kuweka marumaru, na kuhakikisha ujenzi unakuwa na uwiyano katika kila sehemu na kurahisishwa utembeaji wa mazuwaru, sambamba na kuta hizi; kuchukua nafasi ya kuta za zamani zilizo kua zimewekwa kwa muda, zilikua zinawakwaza mazuwaru kutokana na kuanguka anguka hasa katika msimu wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: