Sayyid Adnani Mussawiy akikhutubia kundi la wanawake huko Karachi: Dini ya kiismamu imemwangalia mwanamke kwa jicho la kibinaadamu katika misingi ya usawa na mwanaume

Maoni katika picha
Kufuatia uwepo wa ugeni wa Ataba mbuli tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika matembezi ya misikiti na taasisi mjini Karachi waliyo fanya, walifika katika msikiti wa Imamu Ridhaa (a.s), baada ya mapokezi waliyo pewa na wenyeji, rais wa msafara Sayyid Adnani Mussawiy kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu akapewa nafasi ya kuzungumza, mazungumzo yake aliyaelekeza kwa wanawake wote wa mji wa Karachi walio fika msikitini.

Kwa mujibu wa Maelezo ya Mussawiy aliyotoa kwa mtandao wa Alkafeel, mazungumzo yake yaligusia nukta nyingi, muhimu katika hizo ni:

  • - “Hakika Dini ya kiislamu imemwangalia mwanamke kwa jicho la kibinaadamu katika misingi ya usawa na mwanaume, imemuheshimu na kumtukuza, tofauti na Dini zingine au jamii zinazo mwangalia kama mwanamke tu na raia basi, katika uislamu hakuna tofauti kati ya mwanamke na mwanaume wote ni binaadamu sawa.
  • - Qur’ani tukufu imetaja mifano mingi ya wanawake watukufu, na imeendelea kuwapigia mfano kwa wanaume na kwa waumini kutokana na utukufu wao kiroho, kama vile Asia bint Hizaam na Maryam bint Imraan pamoja na wengine.
  • - Dini ya kiislamu umemsisitiza mwanamke kuvaa hijabu na kujistiri, mnatakiwa kushikamana na vazi hilo na mumfanye bibi Zaharaa na mwanae Aqilah kuwa kiigizo na taa lenu.
  • - Mwanamke wa leo kutokana na utukufu aliopewa katika Dini ya kiislamu anaweza kutengeneza kizazi cha Mitume na wasichana wenye kujiheshimu na wanaotambua mazingira yanayo wazunguka”.

Akaendelea kusema: “Tulizungumzia na mambo yanayo husu ndoa na nyumba upande wa mwanamke hususan katika jamii tunazoishi, na mwisho tukajibu maswali kutoka kwa wasikilizaji kuhusu hukumu za kisheria na maisha ya kijamii”.

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimetuma wawakilishi wao Pakistani katika mji wa Karachi, kutokana na kuwepo kwa mawasiliano baina yao na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), ugeni huo ulikua na ratiba nyingi, ikiwemo kutembelea taasisi za Dini na kijamii pamoja na baadhi ya misikiti na Husseiniyya, pamoja na mambo mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: