Idara ya umeme chini ya kitengo cha uhandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu imefunga taa (57) zenye mwanga mkali na mzuri

Maoni katika picha
Idara ya umeme chini ya kitengo cha uhandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu imefunga taa (57) zenye mwanga mzuri, kwenye nguzo ndefu zinazo lingana na urefu wa jengo la haram ya Abbasi (a.s), kuanzia upande wa mlango wa Kibla ya Abbasi (a.s) hadi katika mlango wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s).

Kiongozi wa idara ya umeme katika kitengo tajwa Mhandisi Ali Hussein Khaffaaf ameuambia mtandao wa Alkafeel sifa muhimu za taa hizo kua: “Taa zilizo fungwa hivi karibuni zinasifa zifuatazo:

  • 1- Ni aina bora na hudumu kwa muda mrefu, zinawarantii wa kudumu miaka mitano.
  • 2- Zinamwanga zaidi ya mara (20) ya taa za kawaida.
  • 3- Zinawaka haraka sana baada ya kuwashwa, tofauti na taa za kawaida ambazo huchukua kati ya dakika mbili hadi tatu kuwaka.
  • 4- Zinatumia umeme mdogo sana, chini ya asilimia (70) ya taa za kawaida.
  • 5- Taa hizi ni rafiki wa mazingira, hazina gesi mbaya, tofauti na taa za kawaida ambazo zina aina nyingi za gesi zenye sumu”.

Kuhusu sehemu zilipo fungwa amesema kua: “Zimefungwa kwenye nguzo zenye urefu wa mita (13), umbali wa nguzo moja hadi nyingine ni mita (25) hadi (30), idadi ya taa zilizo fungwa katika kila nguzo zinatofautiana kutokana na mahitaji ya sehemu husika, nguzo yenye taa chache zaidi inataa mbili, na yenye taa nyingi zaidi ina taa sita”.

Tunapenda kuwafahamisha kua idara ya umeme chini ya kitengo cha uhandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu imesha fanya miradi mingi ya umeme inayo husu Ataba tukufu, ndani na nje ya uwanja wa haram tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: