Miongoni mwa mafanikio yaliyo patikana na yanayo endelea kupatikana katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika upasuaji wa aina mbalimbali wanao fanya, jopo la madaktari bingwa wa kiiraq wamefanikiwa kufanya upasuaji wa aina ya pekee, upasuaji wa kubadilisha sauti, kutoka sauti ya kike na kua sauti ya kiume kwa kijana mwenye umri wa miaka ishirini kutoka katika moja ya mikoa ya Iraq.
Upasuaji huo umefanywa na jopo la madaktari likiongozwa na daktari bingwa wa maradhi ya pua, sikio na koo katika hospitali hiyo Dokta Naadhim Amraan, upasuaji huo umefanyika baada ya vipimo kuonyesha kunatatizo katika koo lake linalo pelekea kubana sauti.
Upasuaji huu umeonyesha mafanikio makubwa katika hospitali ya rufaa Alkafeel, mafanikio haya yanatokana na taufiqi ya Mwenyezi Mungu na uwezo mkubwa walio nao madaktari wa hospitali hii wa kigeni na wazalendo, pamoja na vifaa tiba bora na vya kisasa vilivyopo hospitalini, sambamba na idara nzuri inayo simamia utendaji kwa makini.
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel tembelea toghuti ya hospitali ifuatayo: www.kh.iq au piga simu namba: (07602329999 / 07602344444).