Miongoni mwa ratiba yake ya kujenga mahusiano baina ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika jamhuri ya Pakistan na Ataba tukufu za Iraq, ugeni kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya uliopo katika mji wa Karachi umefanya ziara kadhaa katika vituo vya Dini na utamaduni vilivyopo katika mji wa Karachi pamoja na misikiti na Husseiniyyaat, miongoni mwa ziara hizo ni ziara ya msikiti wa (Sharikatul Hussein –a.s-), ambao ni moja ya misikiti mikongwe na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hukutana hapo na kufanya ibada zao pamoja na kuswali swala za jamaa na harati zingine.
Ziara hii imefanyika baada ya kupata wito kutoka kwa kiongozi mkuu wa msikiti huo kwa wageni kutoka Ataba mbili tukufu, kufuatia maelezo ya mkuu wa msafara Sayyid Adnaan Mussawiy kutoka kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu ambaye amesema kua: “Tumealikwa na kiongozi mkuu wa masjid Sharikatul Hussein (a.s) katika mji wa Karachi kuja kutembelea msikiti huu mtukufu, tumepokelewa vizuri na viongozi wa msikiti huu pamoja na waumini wengi waliokusanyika kwa ajili ya kutupokea”.
Akaongeza kua: “Tulitumia fursa hiyo kumzungumzia bi Zainabu (a.s), msikiti huu umepewa jina hilo ukimkusudia bi Hauraa Zainabu (a.s), tukazungumza machache kuhusu historia yake, elimu yake, uchamungu wake na nafasi kubwa aliyo nayo katika harakati ya Husseiniyya hasa baada ya tukio la Twafu”.
Akaendelea kusema: “Tulizungumza pia kua elimu imegawanyika sehemu mbili: ya kimaumbile na ya kusoma, bi Hauraa Zainabu (a.s) alikua na elimu zote mbili, alikua na elimu ya kimaumbile kwa sababu alikua miongoni mwa walioteuliwa na Mwenyezi Mungu kwani ni mjukuu wa mbora wa viumbe na mtoto wa mbora wa wanawake wa ulimwenguni, na elimu ya kusoma, hakika alisoma kwa watu watukufu zaidi ambao ni maimamu watakasifu na baba yake kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib na ndugu zake Hassan na Hussein (a.s)”.
Waumini waliokusanyika msikitini baada ya swala ya jamaa iliyo swalishwa na Sayyid Adnaan Mussawiy na kutoa mawaidha, waliuliza maswali ya kisheria na kifiqhi. Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimetuma ujumbe katika mji wa Karachi Pakiatan kajika jimbo la Lahoor na Karachi, kufuatia ratiba yake ya kuwasiliana na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), ratiba hiyo ilikua na vipengele vingi, moja ya vipengele hivyo ni kutembelea taasisi za Dini pamoja na misikiti na Husseiniyyaat, pamoja na mambo mengine.