Haya ndio yaliyo semwa na Dokta Shekh Munjidi Ka’abiy katika nadwa ya Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya imeandaa nadwa kupitia tawi lake la wilaya ya Hindia, nadwa hiyo imefanyika katika Maahadi ya ufundi ya Karbala/ kitengo cha uhasibu chini ya anuani isemayo: (Qur’ani na uhai).

Nadwa hii ni miongoni mwa miradi ya maahadi iitwayo (Miradi ya Qur’ani) inayo fanywa katika vyuo vikuu na Maahadi za hapa Iraq, mtoa mada wa nadwa hii alikua ni Dokta Munjidi Ka’abiy, mwenye shahada ya udaktari (phd) katika historia na tamaduni za kiislamu, ameongelea mada tajwa hapo juu (Qur’ani na uhai), ameelezea kuenea kwa utamaduni wa kiislamu na sheria zake zilizo fundishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w), na namna uislamu ulivyo eneza amani katika jamii za wakati huo, akabainisha namna uislamu wa Mutume Muhammad (s.a.w.w) ulivyo fundisha misingi imara ya elimu, akatolea ushahidi surat Alaq, pale Mwenyezi Mungu alipo sema: soma (Iqra-a), hii inamaanisha kua hakuna njia nyingine ya kutafuta mafanikio kwa mwanaadamu zaidi ya kusoma.

Baada ya hapo Shekh Ka’abiy akazungumzia mambo yasiyo faa wanayo kumbana nayo vijana wetu wa sasa, ikiwa ni pamoja na wingu la mitandao ya mawasiliano ya kijamii, namna inavyo poteza wakati wa vijana na kuwafanya wasinufaike na muda, pia akafafanua namna Qur’ani tukufu inavyo fafanua misingi muhimu katika maisha ya mwanaadamu na kuishi kwa amani pamoja na kujiepusha na kila kitu cha kupita, huku akitolea ushahidi matukio mbalimbali ya kihistoria yaliyo tokea katika umma wa kiislamu.

Akamaliza kwa kuwapa nasaha wanafunzi waliohudhuria na kujibu maswali yaliyo ulizwa mwishoni mwa nadwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: