Ugeni wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wakutana na kundi la waumini wa Karachi na wawaambia kua hisia za mapenzi yenu zinatokana na nia nzuri mliyo nayo

Maoni katika picha
Ziara za ugeni wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinaendelea katika mji wa Karachi nchini Pakistan, wanaangalia mazingira ya waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika mji huo, hivi karibuni ugeni huo umetembelea msikiti wa Sayyidu Shuhadaa (a.s), ambao ni miongoni mwa misikiti muhimu sana na wenye harakati nyingi za kidini na kitamaduni, na kukutana na kundi kubwa la waumini katika msikiti huo.

Kiongozi wa msafara huo Sayyid Adnaan Mussawiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumetembelea msikiti wa Sayyid Shuhadaa (a.s) katika mji wa Karachi nchini Pakistan, tukiwa ni wenye kuitikia mwaliko tuliopewa na viongozi wa msikiti huo, tumepata mapokezi mazuri kutoka kwa waumini wa msikiti huo, kisha tukapewa nafasi ya kuzungumza ndani ya msikiti, kwanza tukawafikishia salamu za viongozi wakuu wa kisheria wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai na Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), tukawaambia kua tunafuraha kubwa kuwa pamoja nao katika mkutano uliojaa upendo na kuwafuata maimamu wa Ahlulbait (a.s), hisia za upendo uliopo zinatokana na nia njema yenye msingi mzuri”.

Katika mada yetu tukazungumzia: “Heshima kubwa aliyo nayo mpenzi wa Ahlulbait katika nyoyo za Maimamu watakasifu (a.s), kufuatia kauli ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) kwa mmoja wa maswahaba wake: (Kadhalika wallahi shia wetu wameumbwa kutoka na nuru ya Mwenyezi Mungu na kwake ndio marejeo yao, wallahi mtakutana na sisi siku ya kiyama na sisi tutakuombeeni shufaa, wallahi tutakuombeeni shufaa na mtapata shufaa, kila mtu katika nyie ataonyeshwa moto upante wake wa kushoto na pepo upande wa kulia, wapenzi wake wataingizwa peponi na maadui wake wataingizwa motoni”.

Akaongeza kua: “Katika mazungumzo yetu tukawaambia kua; furaha na huzuni wanazo zipata wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s) ni kielelezo cha yanayo ingia katika nyoyo za maimamu wetu watakasifu, haya yalisemwa na bwana wa mashahidi kumwambia mmoja wa wafusia wake, aliye mwambia: (Mimi hufurahi na kuhuzunika bila kutambua sababu), Imamu (a.s) akamjibu kua: (Hakika huzuni na furaha hufika kwenu kutoka kwetu, sisi tukifurahika au kuhuzunika na nyie mtafurahi au kuhuzunika kwa sababu sisi na nyie tunatokana na nuru ya Mwenyezi Mungu mtukufu, udongo wetu na udongo wenu ni mmoja, udongo wenu ungeachwa kama ulivyo kua mngekua sawa sisi, lakini udongo wenu ulichanganywa na udongo wa adui zenu kama sio hivyo msingetenda dhambi kabisa).

Baada ya kumaliza kutoa mawaidha swala ikakimiwa na kuswalishwa na Sayyid Adnaan Mussawiy rais wa ugeni kutoka Ataba mbili tukufu, baada ya swala alizungukwa na waumini kila kona wakiuliza maswali mbalimbali ambayo aliyajibu vizuri, mwisho wa ziara waumini waliwaomba wageni wawafikishie dua zao kwa bwana wa vijana wa peponi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: