Vipengele muhimu alivyo zungumzia Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa

Maoni katika picha
Katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (27 Rabiul Aakhar 1440h) sawa na (4 Januari 2019m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai (d.i), Marjaa Dini mkuu amezungumzia vipendele vingi vya kimaadili na kijamii, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

 • - Kuna mambo katika jamii yanatishia mmomonyoko wa maadili na kuishi kwa amani.
 • - Tunapo sema heshima ya mtu tunamaanisha hadhi yake katika jamii au kundi fulani inayotokana na mwenendo wake wa dini, utamaduni, tabia na mazingira yake kiuchumi na kisiasa au utu wake bila kujali mambo hayo.
 • - Mwanaadamu ni kiumbe aliyekirimiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu na akafanywa kua bora kushinda viumbe wengine.
 • - Kimaumbile mwanaadamu anahitaji kushirikiana na watu katika maisha yake.
 • - Kuvunjiana heshima kunapingana na maumbile ya kibinaadamu.
 • - Kila mmoja wetu anahitaji kushirikiana na watu wengine kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya kimaisha.
 • - Kuvunja heshima ya mtu kunatokana na ukosefu wa dini, tabia na utamaduni.
 • - Kuvunjiana heshima kunaweza kufanywa na watu wachache itakapokua jamii inakemea swala hilo.
 • - Kuvunjiana heshima kunapingana na dini, tabia njema, mazowea na utu.
 • - Kuvunjiana heshima ni hatari zaidi kutakapokua ni jambo la kawaida katika jamii.
 • - Athari za kuvunjiana heshima huangamiza jamii pale itakapokua ndio tabia ya watu wengi au ikafanywa na kundi la dini au jamii fulani.
 • - Kwa mujibu wa riwaya, kuvunjiana heshima ni kumdharau muumini au kutweza utukufu wake na heshima yake.
 • - Ni kosa kubwa kumvunjia heshima mtu kwa aina yeyote ile.
 • - Tunadhani kumvunjia heshima mtu kua ni jambo dogo, siku ya kiyama tutajua ukubwa wake.
 • - Tunatakiwa kuwa makini tunapoongea au kuandika.
 • - Mada ya kuvunjiana heshima ni ndefu sana tunatakiwa kua makini na kuizingatia kwa sababu inatishia ustawi wa jamii na kuishi kwa amani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: