Kamati ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kusaidia wakazi wa miji iliyo kombolewa kutoka kwa magaidi wa Daesh

Maoni katika picha
Kamati ya ustawi wa jamii chini ya kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, bado inaendelea na majukumu yake japkua vita dhidi ya magaidi wa Daesh imesha isha, wairaq walipata ushindi mkubwa dhidi ya adui huyo aliyetaka kupasua taifa hili na kudhalilisha maeneo yake matukufu, kazi zake imezigawa sehemu nyingi, kuna wanaohusika na wapiganaji wa jeshi la serikali na wa kujitolea katika vikosi tofauti, na wengine wanahusika na kudumisha mawasiliano pamoja na wakazi wa miji iliyo kombolewa kutoka katika udhibiti wa Daesh, na hili ndio walilo fanya hivi karibuni, walipo tembelea miji iliyokombolewa kutoka katika udhibiti wa Daesh katika mikoa ya (Nainawa, Swalahu Dini, Karkuuk na Diyala), kwa ajili ya kusikiliza matatizo yao na kuimarisha uhusiano ili kulinda ushindi uliopatikana kutokana na damu tukufu za walioitikia fatwa tukufu ya kujilinda.

Kiongozi wa msafara na rais wa kitengo hicho Shekh Haidari Aaridhwiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ziara hii ni sehemu ya mfululizo wa ziara nyingi tulizo fanya na tunazo endelea kufanya, chini ya ratiba maalumu inayo husu miji yote iliyo kombolewa kutoka katika udhibiti wa magaidi wa Daesh au iliyo simama imara dhidi ya Daesh, ziara yetu ya sasa imehusisha mikoa minne, hasa miji iliyo kombolewa kutoka katika udhibiti wa Daesh, tumetembelea mkoa wa Diyala katika miji ya (Abbaarah, Bahraz, Hudaida na mji wa Jawadu Bashu), kisha tukaenda katika mkoa wa Swalahu Dini, tukatembelea (kijiji cha Aali Buhasaan, Aali Butufaah, Aali Buaaswi na kijiji cha Aali Buhathma katika mji wa Yathriba), kisha tukaenda katika mkoa wa Karkuuk, tukatembelea mji wa (Aamirliy), kisha tukamalizia ziara yetu katika mkoa wa Mosul, kwenye mji wa (Sanjaar na Bartwala).

Akabainisha kua: “Wakati tukiwa katika miji hiyo tumefanya mikutano mbalimbali, tumeongea na wananchi pamoja na viongozi, tumewahusia kuimarisha amani na usalama, pamoja na kuwafikishia salamu kutoka kwa Marjaa Dini mkuu na watumishi wa Ataba tukufu, sambamba na mambo mengine mengi ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari kwa kufuatilia mienendo yenye utata wa kuamsha fitna za Daesh, na kuhimiza kujenga kuaminiana na kubadilishana taarifa kati ya wananchi na askari, nakusisitiza umuhimu wa wananchi katika kulinda nchi na umoja wa taifa, na kutambua kua Iraq ni hema linalo tufunika wote”.

Akamaliza kwa kusema: “Tuligawa zawadi za tabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakazi wa miji tuliyo tembelea walitupokea kwa furaha kubwa sana, na walituaga vizuri wakiwa na matarajio ya kuwatembelea tena siku zingine”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hutuma misafara ya kwenda kutoa misaada ya hali na mali kwa vikosi vyote vya askari wa serikali na Hashdi Sha’abi, pamoja na kuunda kamati maalumu kwa ajili ya kusaidia familia za mashahidi na kufuatilia hali za majeruhi sambamba na kuweka utaratibu wa kudumisha mawasiliano na wakazi wa miji iliyokombolewa kutoka katika udhibiti wa Daesh au ile iliyo simama imara na ikapambana na Daesh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: