Sayyid Adnaan Mussawiy azungumza na ndugu wa mashahidi wa Karachi nchini Pakistani: Shahada kwa mpenzi na mfuasi wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s) ni uhai, hawajali kama watapata umauti au hawatapata

Maoni katika picha
Sayyid Adnaan Mussawiy kutoka katika kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu na rais wa ugeni wa Ataba mbili tukufu uliopo Pakistani amesema kua; wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanaofuata mwenendo wao hawaogopi kufa, kwao kufa ni uhai, wanacho kiigizo chema kwa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hawajali kuuwawa au kupona, wamehitimu madrasa hiyo na kuna ushahidi mwingi, miongoni mwa ushahidi huo ni Iraq ambayo imetoa mashahidi wengi kwa ajili ya kukomboa ardhi yao.

Ameyasema hayo katika mazungumzo aliyo fanya na ndugu wa mashahidi wa Karachi ndani ya moja ya misikiti ya mji huo, ndugu wa watu walio uwawa kutokana na mashambulizi ya kigaidi, baada ya kuwapa pole akawaambia kua hakika hilo ni jambo tukufu na fahari kwao.

Akamalizia mazungumzo yake kwa kusoma beti zilizo kumbusha msiba wa Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mambo yaliyo tokea katika tukio la Twafu, na namna Abulfadhil Abbasi alivyo kua masaada mkubwa kwa Imamu na ndugu yake (a.s), na namna alivyo watoa ndugu zake pamoja na nafsi yake kwa ajili ya Dini tukufu ya uislamu, akiwa ni mwenye kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu na kutii amri ya Imamu wa zama zake (a.s).

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimetuma ujumbe katika jamhuri ya Pakistan kwenye jimbo la Lahoor na Karachi, kutokana na harakati za kuwasiliana na wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), ziara hiyo ilikua na vipengele vingi, kikiwemo kipengele cha kutembelea taasisi za Dini, misikiti na Husseiniyya, ziara hizo zilipambwa na mambo mengine mengi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: