Taa mpya zang’arisha kuta na paa la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kukamilika kwa kazi inayofanywa na idara ya umeme chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi ya ukarabati na ufungaji upya wa mtandao wa umeme katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s). Hivi karibuni zimebadilishwa taa za ndani ya haram tukufu, zimefungwa taa zenye mwanga mzuri na rangi za kupendeza, zinazo endana na nakshi zilizopo pamoja na mwanga wa taa za mapambo.

Mtandao wa Alkafeel umekutana na kiongozi wa idara, Mhandisi Ali Abdulhussein Abbasi ambaye ametuhadithia kuhusu kazi hiyo kua: “Kazi ya kufunga taa katika haram tukufu imehusisha kutoa taa za zamani na kuweka mpya kwa kuangalia kiasi cha mwanga unaohitajika”.

Akaongeza kua: “Kazi hii ilitanguliwa na kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kubaini kiwango cha mwanga unaohitajika, kisha tukaweka nyaya za umeme, halafu tukafunga taa zenye uwezo tofauti kulingana na sehemu ya kila taa, pia tumefunga taa za aina tofauti na maumbo tofauti, korido zinazo zunguka haram tukufu zimefungwa jumla ya taa (548) zenye mianga tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: