Katika juhudi zake endelevu za kutoa malezi bora kwa wanafunzi, na kuwahifadhisha kitabu cha Mwenyezi Mungu kitukufu, shule ya msingi Saaqi imewapa zawadi wanafunzi wa shule za Al-Ameed ambazo zipo chini ya Atabatu Abbasiyya walio hifadhi Qur’ani tukufu.
Zawadi zinawapa moyo wa kuendelea kuhifadhi Qur’ani tukufu, wamefanyiwa mahafali maalum na kutembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakiwa na viongozi wao, ziara hiyo inawajenga kiimani na kuwashajihisha kuendelea kuhifadhi sura nyingi zaidi za Qur’ani, kwa mujibu wa maelezo ya Ustadhat Samiyya Karim kutoka katika shule ya Saaqi.
Akaongeza kua: “Hafla yao ilihusisha tamasha lililo fanywa ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kabla ya tamasha hilo tulifanya kisomo cha Qur’ani, tukamalizia ratiba katika mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kutabaruku na ukarimu wa mwezi wa bani Hashim”.
Tunapenda kufahamisha kua shule za Al-Ameed ambazo zipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu zinaendelea kutoa mafunzo mbalimbali na kufanya warsha na semina kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na maarifa ya Dini kwa wanafunzi wake.