Kwa picha: Uwekaji wa marumaru ya kwanza katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wanaofanya kazi katika mradi wa kuweka marumaru kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wameanza kuweka marumaru ya kwanza katika sehemu ya kwanza ya mradi huo, sehemu iliyopo katikati ya mlango wa Imamu Ali Haadi (a.s) na mlango wa Furaat (Alqamiy), baada ya kukamilisha maandalizi ya kazi hiyo, kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi Majidi Swaaigh rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu: “Kazi hii inafanywa sanjari na kuweka marumaru katika jengo ambayo umepiga hatua kubwa kwa sasa”.

Akasema: “Tunaweka marumaru ya kifahari zaidi, na tunatumia njia ya kitaalamu inayo zifanya kua imara zaidi, na kuzifanya ziishi kwa muda mrefu pia zinaendana na marumaru zilizopo katika jengo, ili kuweka uwiyano wa kiufundi na kihandisi”.

Akabainisha kua kazi ya kuweka marumaru imegawanywa katika hatua, kila hatua ina sehemu yake, kabla ya kugawa hatua hizo tulifanya upembuzi yakinifu na kubaini mahitaji pamoja na kuweka mikakati ya utendaji, pia tuka ainisha nakshi na mapambo yanayo endana na sehemu zingine za Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Kazi za awali zilizo fanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, zilihusisha vitu vingi miongoni mwake ni:

  • - Kuondoa marumaru za zamani.
  • - Kuondoa baadhi ya sehemu za zege za zamani na kurekebisha sehemu zilizo athirika.
  • - Kurekebisha sakafu na kuziba sehemu zilizo pasuka kwa kutumia vifaa maalum.
  • - Kumwaga zege jipya lenye viwango maalumu litakalo saidia ukaaji wa marumaru juu yake na kuondoa unyevunyevu.
  • - Kutengeneza tabaka la chuma na kuliweka chini ya zege.
  • - Kutengeneza mtandao wa kusambaza maji, mawasiliano, tahadhari na zima moto pamoja na kuunganishwa na mtandao mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kuhusu wasifu wa marumaru amesema kua: “Marumaru hizi ni za kawaida lakini ni adimu sana (Malt Oksi), zinasifa nyingi, miongoni mwa sifa zake, marumaru ni za kawaida zenye rangi nzuri na imara, zinauwezo mkubwa sana wa kuvumilia mazingira ya hali ya hewa, zinamuonekano mzuri, zina unene wa (sm 4) takriban”.

Kumbuka kua mradi wa kuweka marumaru katika sakafu ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ni mradi unaokamilisha miradi iliyo tekelezwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, unatekelezwa kutokana na kuharibika kwa marumaru zilizo kuwepo jambo lililokua linaharibu muonekano wake pia ukizingatia na ukongwe wa marumaru hizo, kwani zina zaidi ya miaka (50), kwa hiyo uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeona ni muhimu kubadilisha marumaru hizo, kwa ajili ya kuongeza uzuri wa muonekano wa sehemu hii ambayo ni miongoni mwa sehemu za peponi, kwa namna ambayo itafurahisha nyoyo za mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: