Atabatu Abbasiyya tukufu imemaliza kutengeneza kituo cha kusambaza maji katika wilaya ya Shatul Arabu

Maoni katika picha
Kikosi kilicho tumwa na Marjaa Dini mkuu katika mji wa Basra kutatua tatizo la maji, bado kinaendelea kufanya kazi chini ya mkakati maalum, Atabatu Abbasiyya tukufu inamchango wake katika kazi hizo, imejukua majukumu kadhaa yatakayo punguza tatizo la maji katika wilaya ya Shatul Arabu, kutengeneza kituo cha (R.O station), kwa ajili ya kusambaza maji.

Msimamizi wa kazi hii rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi ya Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu umuhimu wa kituo hicho, amesema kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua majukumu matatu muhimu, miongoni mwa kazi zinazo fanywa na jopo la wataalamu waliotimwa na Marjaa Dini mkuu kuja kusaidia utatuzi wa tatizo la maji, miongoni mwa majukumu hayo ni kutengeneza kituo cha kusambaza maji katika vijiji vya wilaya ya Shatul Arabu, tumekodi ardhi yenye ukubwa wa (2m1000) na kujenga mradi huu juu ya ardhi hiyo, mradi huu (R.O. station) unauwezo wa kuzalisha lita (30,000) kwa saa.

Akaongeza kua: “Mradi unahusisha mitambo ya kusafisha maji yenye ubora mkubwa wa kimataifa (mitambo ya kusukuma maji imetengenezwa Itali na vifuniko vyake vimetengenezwa Marekani na vifaa vingine vimetengenezwa India pamoja na ubao wa ulinzi na kugawa umeme umetengenezwa Uswisi na vitu vingine kutoka sehemu mbalimbali), pamoja na kuweka (R.O) mahodhi ya maji safi yasiyo safishwa na mahodhi ya maji safi yaliyo safishwa na kua tayali kwa kunywa, na kupajengea paa huku sakafu ikiwa na kina cha (sm20), kuta zake zimetengenezwa kwa vipande vya Sandawiji huku paa yake ikiwa imejengwa kwa chuma, pamoja na kuweka dari na kufunga taa za ndani na nje”.

Pia kuna mitambo ya (exhaust system), akaendele kusema kua: “mradi huu umefungwa mtambo wa kuvuta maji, unaoweza kufanyiwa mabadiliko yoyote kutokana na maendeleo yatakavyo ruhusu siku za mbele, unaweza kubadilika kutokana na maendeleo yeyote yanayo weza kufanyika, mradi huu umewekewa tahadhari za kiufundi kutokana na namna ulivyo sanifiwa na kituo cha utafiti Alkafeel, na watekelezaji wa mradi ni shirika la kiiraq Twaairu Thalji”.

Akabainisha kua: “Tumethibitisha kazi zilizo kamilika kua zimeendana na mchoro tuliokubaliana sambamba na kulingana vifaa vya ndani ya eneo la mradi pamoja na vifaa vya ulinzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: