Miongoni mwa mambo yanayo pewa umuhimu mkubwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya ni kuandaa kundi la wahifadhi Qur’ani, na imepiga hatua kubwa katika swala hilo, inaidara maalumu iitwayo (Idara ya kuhifadhi Qur’ani) inajukumu la kuhifadhisha Qur’ani kwa viwango tofauti.
Kwa ajili ya kuimarisha waliohifadhi Qur’ani na kuwaandaa kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, idara ya kuhifadhisha Qur’ani imeandaa mashindano wa maandalizi (kuwapima) wanafunzi wanaohifadhi, shindano hilo linaangalia (Uwezo wa kuhifadhi, hukumu za usomaji, kusimama na kuanza katika usomaji, sauti na naghma) wanashiriki zaidi ya wanafunzi (120) chini ya jopo la majaji walio bobea katika maswala ya Qur’ani, kila mshiriki anashiriki kulingana na kiwango chake, wamegawiwa katika vikundi, kila mmoja na idadi ya juzuu alizo hifadhi hadi wale walio hifadhi Qur’ani yote, watashindana kwa makundi kulingana na tabaka zao.
Kiongozi wa idara ya kuhifadhi katika Maahadi, Ustadh Hamza Fatalawiy amesema kua: “Washiriki wana ari mkubwa sana katika shindano hili la Qur’ani tukufu, shindano hili ni la kujipima uwezo kuna mashindano mengine yataandaliwa, tumeandaa mazingira mazuri yanayo wawezesha wanafunzi kuhifadhi Qur’ani kwa urahisi, kuna chakula kizuri, michezo inayo komaza akili na safari za kitalii, kwa ajili ya kuonyesha utukufu wao kwani wamebeba kitabu cha Mwenyezi Mungu katika nyoyo zao, mashindano haya yameandaliwa kwa ajili ya kuimarisha uwezo wao na kuwaandaa kushiriki mashindano ya kitaifa na kimataifa”.