Kutokana na maelezo ya wahandisi wa Atabatu Husseiniyya tukufu waliotekeleza mradi huo kwa mtandao wa Alkafeel, mradi huu unasifa zifuatazo:
- - Eneo lililo ongezwa katika eneo la zamani linaukubwa wa 2m (2215) baada ya kuongeza eneo la shule ya Sajjaad (a.s) iliyo jirani yake.
- - Kuwekwa paa katika Mukhayyamu Husseiniy yenye ukubwa wa (2m2200).
- - Mukhayyamu umekua na tabaka tatu kwa ajili ya kupokelea mazuwaru, na unamigahawa miwili, wa wanaume na wanawake, pamoja na eneo la uwanja ndani ya Mukhayyamu.
- - Mukhayyamu umepauliwa hema tano zenye ukubwa wa (mt10x10), pamoja na hema kubwa mkabala na mlango mkuu wa kuingia, nalo litaitwa hema la Imamu Hussein (a.s).
- - Mahema yote yamenakshiwa na kuwekwa mapambo mazuri ya dhahabu pamoja na aya za Qur’ani tukufu, kila hema linamadirisha (12) takriban, madirisha ya hema kubwa yanaukubwa wa (mt2).
- - Limeondolewa dirisha la mbao lililo kuwepo latika hema la Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya Mukhayyamu Husseiniy na kuwekwa dirisha lililo tengenezwa kwa dhahabu na fedha.
- - Kupanuliwa sehemu ya mahema manne maalumu ya Imamu Hussein na familia yake, ambayo ni; hema la Imamu Hussein (a.s), hema la Imamu Zainul-Aabidiin (a.s), hema la Hauraa Zainabu (a.s) na hema la Qassim (a.s).