Semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa uhazini katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuboresha uwezo wao wa kazi na kuwafanya waendane na maendeleo yaliyopo katika sekta ya uhazini, kitengo cha uhazini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeratibu semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa uhazini wanaofanya kazi katika vitengo mbalimbali vya Ataba tukufu.

Kuhusu semina hii tumeongea na mkufunzi wa semina na kiongozi wa idara ya mipango ya kielimu na uhazini katika kitengo cha uhazini Ustadh Ahmadi Muhsin Jaasim, amesema kua: “Hii ni semina ya tano kuhusu masomo haya, inahusisha watu wanaofanya kazi katika ofisi za uhazini kwenye vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya, wameshiriki watu kutoka kitengo cha (tarbiyya na taaliim) na kitengo cha (maa baina haramaini) na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) pamoja na watumishi wapya wa vitengo vya uhazini, na vitengo vingine vinatarajiwa kujumuishwa katika semina zijazo Insha Allah”.

Akaendelea kusema: “Semina itachukua siku tano, kila siku wanakaa darasani kwa muda wa saa tatu kwa masomo mawili, wanafundishwa njia za maandalizi ya kutunza kitu zinazo tumika katika uhazini, kuanzia kubaini kinacho taka kutunzwa hadi usanifu na upangiliaji wa sehemu, kisha tunamalizia na namna ya kukagua nyaraka za kuingiza na kutoa vitu, mwisho wa semina tutawapa mtihani wa kupima uwelewa wao”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hutoa mafunzo ya kujenga uwezo kwa watumishi wake wa vitengo na idara mbalimbali na kwa viwango tofauti, ili kuwapa uwezo na mbinu mpya zinazo wawezesha kuboresha utendaji wao katika sekta mbalimbali ndani na nje ya Ayaba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: