Multaqal Qamaru yatumia siku za mapumziko za mwisho wa wiki kutoa mafunzo ya kimaadili

Maoni katika picha
Kunufaika na mapumziko ya mwisho wa wiki na kwa ajili ya kufundisha maadili mema kwa wanafunzi, kituo cha Multaqal Qamaru cha kiutamaduni kinatoa mafunzo mbalimbali ya kimaadili, ni mafunzo ya kielimu na kitamaduni mahsusi kwa vijana wa tabaka tofauti, yanalenga kuwawezesha kupambana na changamoto za kidini, kitamaduni na kijamii, bila kutumia chuki wala jazba, mambo ambayo huleta madhara katika jamii, mafunzo hayo yanasimamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ustadh Ali Badriy mmoja wa wajumbe wa Multaqa ameuambia utandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Kwa ajili ya kuhakikisha tunanufaika na kila dakika ya mapumziko tunayo weza kutoa mafunzo kwa vijana watu na walimu, pamoja na watu wengine katika jamii, kituo cha Multaqal Qamaru kinatoa mafunzo siku ya Ijumaa na Jumamosi kila wiki, chini ya ratiba makini inayo endana na umri wa washiriki pamoja na kutofautiana kwa viwango vya elimu zao, masomo haya yanakamilisha masomo waliyo fundishwa wakati wa likizo za kiangazi, lakini masomo ya sasa yanatofautiana na yale waliyo fundishwa mwanzo, kwani haya yanautangulizi wake, Atabatu Abbasiyya tukufu inagharamia usafiri wao pamoja na malazi yao”.

Shekh Haarith Daahi mkufunzi na kiongozi wa Multaqa amesema kua: “Idadi ya washiriki katika semina ya awali ni (30) kutoka katika shule za mji wa Sha’ala huko Bagdad, wanasoma saa (12) kwa siku mbili ya Ijumaa na Jumamosi, ndani ya ukumbi wa Qassim bun Hassan (a.s), zitafuata semina zingine nyingi hadi washiriki wamalize masomo yao yote yaliyo andaliwa na Multaqal Qamaru, semina hii imekua na mwitikio mkubwa kutokana na umuhimu wa masomo wanayofundishwa kwani yanagusa uhalisia wa maisha yao, masomo haya yalitanguliwa na masomo mengine mengi waliyo fundishwa wakati wa likizo za kiangazi”.

Kumbuka kua (Multaqal Qamaru) ni moja ya harakati za kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya, hutolewa mihadhara mbalimbali na hufanywa warsha na mafundisho tofauti kwa vijana na wanaharakati katika jamii, kwa ajili ya kupambana na fikra potofu na kuwafanya vijana waendane na uhalisia wa mazingira ya kiiraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: