Kuanza maandalizi ya kongamano la tatu la Ruuhu Nubuwwah

Maoni katika picha
Kutokana na mafanikio yaliyo patikana katika awamu mbili za kongamano la kiutamaduni Ruuhu Nubuwwah, rais wa kamati ya maandalizi Ustadhat Bushra Jabbaari Badani ametangaza kuanza maandalizi ya kongamano la awamu ya tatu, ambalo hufanywa katika kumbukumbu ya kuzaliwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) pamoja na kuangalia mchango wake katika dini, jamii na malezi ya familia.

Akaongeza kua: “Hakika maandalizi ya kongamano litakalo anza tarehe ishirini Jamadal Thaani mwaka huu, yamehusisha kuandaa kamati ndogo ndogo zinazo tokana na kamati kuu ya maandalizi, na kugawa majukumu kwa kila kamati, sambamba na kufanya vikao vya kujadili mambo makuuu yatakayo fanyika pamoja na vipengele vyake”.

Akabainisha kua: “Tumesha baini ukumbi tutakao fanyia kongamano, nao ni ukumbi mkuu wa kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s), na tumetuma mialiko kwa watafiti wa kisekula na kihauza kwa ajili ya kuhudhuria na kushuriki katika kuwasilisha mada, pamoja na kuandaa mialiko mingine kwa ajili ya vyombo vya habari, ili viripoti tukio hilo muhimu linalo simamiwa na wanawake wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akasema kua: “Hakika hizi ni juhudi za wakinadada wa kitengo cha Zainabiyyah na idara ya wanawake pamoja na idara ya redio na shule za Al-Ameed pamoja na Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, bila kusahau idara ya kituo cha Swidiiqah na watumishi wake wanaofanya kazi kubwa kuhakikisha kongamano linafanika kwa ufanisi mkubwa”.

Kumbuka kua lengo la kufanya kongamano hili ni kubainisha utukufu wa bibi Zaharaa (a.s) katika nyanja zote, pamoja na kuonyesha nafasi yake katika elimu kupitia tafiti mbalimbali zitakazo wasilishwa, na kuzipatia maktaba nyaraka zinazo mzungumzia mtukufu huyu na athari yake katika elimu na jamii pamoja na kubaini turathi za mbora wa wanawake wa ulimwenguni (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: