Ugeni kutoka wizara ya viwanda na madini ya Iraq umetembelea shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Aljuud

Maoni katika picha
Ugeni kutoka wizara ya viwanda na madini ya Iraq kupitia kamati ya utafiti na maendeleo ya viwanda, umetembelea shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Aljuud ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kuangalia mafanikio yaliyo patikana katika shirika hilo kwenye sekta ya viwanda na kilimo hapa Iraq.

Ugeni huo ulihusisha wakuu wa vitengo na vituo katika vizara ya viwanda na madini, wageni hao wameridhishwa na walicho kiona, na wamesifu kiwango cha uzalishaji unaofanywa na shirika la Aljuud, wakasema uzalishaji huo ni fahari kwa taifa, ugeni umetembelea sehemu mbalimbali za shirika na wakaangalia mitambo na bidhaa zinazo tengenezwa.

Tunapenda kuwafahamisha kua shirika la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa Aljuud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu linamchango mkubwa sana katika soko la Iraq, hususan bidhaa za kilimo na viwanda, limekua kimbilio la wakulima na wenye viwanda hapa Iraq, ukizingatia kua bidhaa zake zinaubora wa hali ya juu, kwani zinatengenezwa kisasa zaidi, na limejikita katika sekta mbili ya kilimo na viwanda.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: