Kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimepiga hatua kubwa katika ujenzi wa bweni za chuo kikuu cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Baada ya kukamilisha ujenzi wa ghorofa la kwanza katika bweni la chuo kikuu cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kitengo cha usimamizi wa kihandisi kimepiga hatua kubwa katika ujenzi wa ghorofa la pili, kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha kihandisi Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi aliyo toa kuuambia mtandao wa Alkafeel: “Mradi huu unajengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1113), umbo la jengo limetengenezwa kwa vyuma, na vyumba vimekatwa kwa tofali za Intalock pamoja na kuskim ukuta pia kuna baadhi ya sehemu zimetumika tofali za block na sehemu zingine ukuta umewekwa mozaiko, bila kusahau sehemu kubwa ya ukuta itawekwa mozaiko sambamba na kufunika dari kwa vifaa maalumu, na kuweka madirisha ya Alminiam na milango ya mbao.

Akaongeza kua: “Katika utekelezaji wa mradi huu umeshuhudiwa ujenzi wa kisasa kabisa, jengo hili linavyumba (36) vya kulala pamoja na vyumba viwili vya kufulia na majiko mawili na sehemu ya vyoo”.

Akaendelea kusema: “Mradi huu unatekelezwa pamoja na mambo yote ya lazima, kama vile mfumo wa umeme na mambo yote yanayo husiana na umeme pamoja na mfumo wa maji taka na maji safi, hali kadhalika umewekwa mfumo wa kamera na Intanet”.

Kuhusu kazi zinazo endelea katika ghorofa la pili na kiwango kilicho kamilika amesema kua: “Hakika kazi inaendelea vizuri inatarajiwa kukamilika kwa wakati, karibu asilimia %60 imesha kamilika na maendeleo ni mazuri”.

Kumbuka kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi ni moja ya vitengo muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kina kazi nyingi sana kama vile kufanya matengenezo katika majengo yeto ambayo yapo chini ya Atabatu Abbasiyya, sambamba na kazi za usanifu na usimamiaji wa miradi mingi inayo fanywa na Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: