Kujibu maswali muhimu yaliyo tokana na ushirikiano wa Atabatu Abbasiyya tukufu na chuo cha Naashitwah: Vipi tutatatua matatizo yetu ya kinafsi? Na furaha ya mtu hupatikana vipi?

Maoni katika picha
(Kwa ajili ya furaha yako na kutatua matatizo yako ya kinafsi..) hiyo ndio anuani ya nadwa ya kielimu iliyo tokana na utafiti wa elimu ya nafsi, jamii na historia, utafiti huo umefanyika kinadhariya na kivitendo, kikao cha nadwa kimefanyiwa ndani ya kitivo cha malezi na elimu za kibinaadamu katika chuo kikuu cha Diyala, kwenye ukumbi wa Allamah Mustwafa Jawaad siku ya Jumatatu (7/1/2019m) na kuhudhuriwa na watu karibu (150), miongoni mwao ni walimu wa chuo pamoja na mkuu wao Dokta Naswifu Jaasim Khafaaji.

Nadwa hii ni sehemu ya harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu inazofanya katika vyuo vikuu vya Iraq, mtoa mada alikua na mtafiti Ustadh Jaasim Muhammad Saidiy mkuu wa kituo cha utamaduni na habari za kimataifa Alkafeel, akajikita katika kuelezea namna ya kupata furaha, neno furaha alilitafsiri kua ni hisia ambazo hupatikana ndani ya mwanaadamu hutokana na sulhu na amani ya ndani baina ya nafsi na akili.

Mtafiti ameelezea mtazamo wake katika kutibu nafsi, akatumia kanuni aliyo iita (fanya kitendo cha kuaga), jitahidi kubaini na kutibu tatizo la kutokua makini na kutotumia akili katika kutafiti au kukumbuka jambo”.

Wakati anajibu baadhi ya maswali akabainisha kua, hakika furaha haipatikani kwa kusikiliza miziki, wala hauwezi kutatua tatizo kwa kutumia dawa za kulevya au kwenda safari ya kitalii (kustarehe), hakika mambo hayo ni sababu ya kuchelewa kutatua tatizo, utatuzi wa tatizo hupatikana kwa nafsi kukiri tatizo lake na kuwepo kwa suluhu kati ya akili na nafsi, nafsi inatakiwa ikiri matatizo yake na kuyabaini kisha kuyawekea utatuzi, ili uweze kutatua tatizo lazima ulielewe kisha ulitafutie utatuzi unaofaa, mtafiti akabainisha aina za matatizo yaliyo tokea siku za nyuma, yanayo tokea sasa na yatakayo tokea siku za mbele, na akaonyesha njia za kuyatatua, washiriki walionyesha kufuatilia kwa karibu sana mada hii, baada ya kumaliza kutoa mada walipewa nafasi ya kuuliza maswali na wakafafanuliwa namna ya kutatua matatizo mengi yanayo wakuta wanaadamu.

Mwisho wa nadwa; mkuu wa kitivo cha malezi na elimu za kibinaadamu Dokta Naswifu Jaasim Muhammad Khafaaji alimshukuru sana mtoa mada, Ustadh Jaasim Muhammad Saidiy, akampa zawadi ya ngao ya chuo na hati ya shukrani.

Kumbuka kua katika ushirikiano uliopo kati ya Atabatu Abbasiyya tukufu na vyuo vikuu vya Iraq, chuo kikuu cha Diyala kimefanya nadwa ya kielimu kuhusu kuandaa utambulisho wa taifa kwa kila mji na nafasi yake katika kujitoa kwenye matatizo, chuo hicho mwaka jana kilialika mtafiti kwa ajili ya kuzungumzia mada ya jamii kwa maendeleo ya taifa la Iraq kama nchi, jamii na dola.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: