Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kitengo kilicho tajwa hapo juu, Ustadh Zainul Aabidina Adnaan amesema kua:
- - Idadi ya mazulia yaliyo tandikwa imefika (750).
- - Kila zulia moja linaukubwa wa mita 3x2.
- - Mazulia yametengenezwa Iran kwa kufuata vipimo maalum vya uwanja wa haram tukufu.
- - Mazuria yanarangi nyekundu yenye nakshi za michoro ya mimea iliyo pambwa vizuri kwa nakshi za kiislamu.
Akaongeza kua: “Tumetandika makapeti mekundu katika milango la haram tukufu katika eneo la mita za mraba (600), kapeti hizo zinaupana wa mita tatu na urefu wa mita (25), kabla ya kutandika tulianza kusafisha na kupiga deki ndani ya haram tukufu”.
Kumbuka kua kitengo cha usimamizi wa haram tukufu kinajukumu la kuisafisha na kutandika mazulia kila baada ya muda fulani, na kuhakikisha wanatunza uzuri wa haram tukufu ya Abbasi na kulinda mazingira ya kiimani anayo yahisi mtu anayekuja kutembelea kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s).