Balozi wa Jamhuri ya watu wa China amesema kua hii sio ziara ya kwanza kwetu, katika juhudi za kuimarisha urafiki kati ya ubalozi wa China na taasisi za Dini za Iraq zikiwemo Ataba tukufu.
Ameyasema hayo katika mazungumzo aliyofanya na mtandao wa Alkafeel wakati alipotembelea Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo Alkhamisi (3 Jamadal Uula 1440h) sawa na (10 Januari 2019m), amesema kua: “Nimekutana na viongozi wa Atabatu Abbasiyya, nitafanyia kazi taarifa nilizo pewa na nyie kuhusu baadhi ya miradi, hususan miradi ya kilimo na viwanda, nitajitahidi kudumisha mawasiliano na kuimarisha uhusiano baina yetu kwa faida ya pande mbili”.
Akaongeza kua: “Hakika jamhuri ya China ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Iraq na inawafanya biashara wengi katika taifa hili, tupo tayali kuendelea kushirikiana kibiashara na Iraq baada ya kuondolewa Daesh, katika mikoa yote na kwenye sekta tofauti”.
Akasisitiza kua: “Hakika mji wa Karbala ni mji mtakatifu na mji muhimu sana katika ulimwengu wa kiislamu unahistoria ndefu, na sisi tunauheshimu sana mji huu, tumefanya juhudi kubwa ya kurahisisha ujio wa mazuwaru kutoka China katika mji mtukufu wa Karbala wakati wa ziara ya Arubaini”.
Akamaliza kwa kusema: “Naushukuru sana uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mapokezi mazuri waliyo tupa, ambayo ni kielelezo cha wazi cha uhusiano mzuri uliopo baina yetu”.
Balozi wa China na ujumbe aliofuatana nao walikutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) aliye elezea miradi mbalimbali inayofanywa na Ataba tukufu.
Mheshimiwa balozi wa china alitembelea korido za Atabatu Abbasiyya akisindikizwa na mjimbe wa kamati kuu ya uongozi wa Ataba tukufu Mhandisi Jafari Saidi Jafari, na akaangalia mradi wa upauaji na upanuzi wa haram tukufu pamoja na mfumo wa viyoyozi na miradi mingine, balozi alifurahishwa na umakini pamoja na utendaji mzuri aliyo uona, akasifu uzuri wa mapambo ya kiislamu na nakshi zilizopo katika kuta na korido za Atabatu Abbasiyya tukufu.
Balozi wa china alihitimisha ziara yake kwa kutembelea makumbusho ya vifaa na nakala kale ya Alkafeel, alifurahishwa na vifaa kale vilivyopo katika makumbusho hiyo tukufu, alisikitishwa alipoona athari za kushambuliwa kwa kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) na nakala kale za msahafu pamoja na vifaa kale vingine vya thamani.