Nukta muhimu alizo zungumzia Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) leo (4 Jamadal Uula 1440h) sawa na (11 Januari 2019m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), amezungumzia nukta nyingi za kimalezi na kimaadili zinazo endana na maisha yetu, miongoni mwa nukta huzo ni:

 • - Familia ndio msingi wa kila mtu.
 • - Kila jamii lazima iwe na misingi ya kuamiliana.
 • - Misingi ya kuamiliana ndio hujenga jamii.
 • - Wakati mwingine wanajamii huwa na upeo mkubwa wa kutambua mambo mengi.
 • - Wakati mwingine familia huwa makini na huwa na watu wasomi na wajuzi wa vitu vingi wanaoweza kutakua matatizo yao wenyewe.
 • - Miongoni mwa matatizo yanayo lalamikiwa na baadhi ya watu ni kukosekana kwa mlezi wa familia katika upande wa kuonesha anaijali na sio upande wa kuihudumia kwa mali.
 • - Kila mambo yanapokua magumu au mepesi katika ulimwengu wa teknolojia familia zinaathirika kwa kutengana au kushikana.
 • - Tunahitaji toknolojia lakini lazima ziendane na majukumu ya baba.
 • - Baba wa familia anatakiwa aonyeshe uwepo wake katika familia.
 • - Kutoa huduma za kipesa kwa familia yako ni jambo zuri lakini usisahau kuwapa huduma za kiroho.
 • - Baba wa familia anajukumu la kiutawala na kimalezi katika familia yake.
 • - Tunatakiwa tujifundishe kwa kiongozi wa waumini (a.s) namna ya kuwajali watoto.
 • - Baba anapokaa na familia yake na kuuliza hali zao, hakika familia hiyo itabarikiwa.
 • - Enyi wakinababa watukufu, familia zenu na watoto wenu wanahaja kubwa na nyie pamoja na kuwanunulia chakula wanatakwa kukuona na kusikia kauli yako.
 • - Ewe baba unauzowefu mkubwa na wewe ni mkubwa kushinda mtoto wako muelekeze namna ya kuingia katika jamii.
 • - Ewe baba fuatilia na ulizia maendeleo ya watoto wako, kumfuatilia mwanao kunamuimarisha na kumfanya atambue kua nyuma yake kuna baba, mama au kaka anaye fuatilia maendeleo yake.
 • - Sote tunawajibika kuhakikisha watoto hawapotei na hawatengani na familia zao.
 • - Ewe baba lazima uongee na mwanao na uonyeshe mapenzi yako kwake.
 • - Sisi sote tunawajibu na watoto wanajua baba ndio mlezi.
 • - Serikali, jamii, taasisi, jumuiya na kila mtu anatakiwa kutekeleza wajibu wake katika familia.
 • - Familia inahitaji uwepo halisi wa mlezi wa familia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: