Mwezi tano Jamadal Uula Dunia ilinawirika kwa nuru ya Aqilat Qubra

Maoni katika picha
Mwaka wa sita Hijiriyya nyumba ya Alawiyya ilipata furaha kwa kuzaliwa mtoto wa tatu miongoni mwa watoto wao, nae ni binti wa kwanza wa Imamu kiongozi wa waumini na bibi Fatuma Zaharaa (a.s), siku ya mwezi tano Jamadal Uula alizaliwa bibi Zainabu (a.s) katika nyumba yenye viumbe bora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, amboa ni: Muhammad Rasuulu Llah, Ali Amirulmu-uminina na Fatuma Sayyidat Nisaail-Aalamina (a.s).

Baada ya kuzaliwa mama yake bibi Zaharaa (a.s) alimpeleka kwa Amirulmu-uminina (a.s), akamwambia mpe jina huyu mtoto, akamwambia siwezi kumpa jina mbele ya Mtume (s.a.w.w), Mtume alipo kuja; Ali (a.s) akamwomba ampe jina mtoto, Mtume (s.a.w.w) akasema: siwezi kumpa jina mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, Jibrilu (a.s) akakaja kwa Mtume (s.a.w.w), akampa salamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kisha akamwambia: mtoto huyu mpe jina la Zainabu, hakika Mwenyezi Mungu amemchagulia jina hilo, kisha Jibrilu akaelezea matatizo yatakayo mpata, Mtume (s.a.w.w) akalia halafu akasema: atakaelia kutokana na matatizo atakayopata binti huyu atakau sawa na atakaewalilia kaka zake Hassan na Hussein (a.s)..

Amekulia katika nyumba ya elimu na maarifa na mashukio ya wahyi na Tanziil, ndio.. aliishi katika shule ya Utume na Uimamu na akahitimu shule hizo, ameishi chini ya uangalizi wa Mtume wa mwisho Muhammad (s.a.w.w) na wasii wake Ali bun Abu Twalib (a.s) na baba wa baba yake Fatuma Zaharaa (a.s), mbora wa wanawake wa duniani na Hassan na Hussein (a.s), mabwana wa vijana wa peponi, na anaye hitimu shule hizo anafaa kupigiwa mfano wa mwanamke boro.

Alikua ni mfano kwa kujihifadhi, Yahya Mazini anasema: nilikua jirani na kiongozi wa waumini (a.s) katika mji wa Madina kwa muda mrefu, nilikua nakaa karibu na nyumba aliyokua anaishi binti yake bibi Zainabu, siku wahi kumuona wala kusikia sauti yake, alikua akitaka kutoka kwenda kwa babu yake Mtume (s.a.w.w) anatoka usiku Hassan akiwa kuliani kwakwe na Hussein kushotoni kwake na Amirulmu-uminina mbele yake, akikaribia kaburi tukufu Amirulmu-uminina (a.s) anapunguza mwanga wa taa, siku moja Hassan (a.s) akamuuliza baba yake kwa nini anafanya hivyo, akamwambia: naogopa watu wasimwangalie dada yako Zainabu, Imamu Hussein (a.s) alikua anapo tembelewa na Zainabu anasimama kwa ajili ya kuonyesha utiifu kwake, alikua anamkalisha sehemu yake. Hakika bibi Zainabu (a.s) alikua shujaa na mfasaha mkubwa, msimamo wake katika ardhi ya Karbala hauelezeki, inatosha kusema kua yeye ndiye aliyekamilisha mapambano ya Imamu Hussein (a.s), maneno yake yalitetemesha arshi za matwaghuti.

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyo kufa na siku atakayo fufuliwa na kuchukua kisasi kwa wale waliomdhulumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: