Wanafuzi wa Madsarat Aswhaabul-kisaa (a.s) wameshiriki katika usomaji wa Qur’ani tukufu ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s) na muendelezo wa kuhifadhi Qur’ani tukufu, katika mradi wa Arshu Tilaawah unaofanywa kila wiki ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kituo cha miradi ya Qur’ani kilicho chini ya Maahadi ya Qur’ani ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimealika Madrasat Aswhaabul-kisaa (a.s) ambayo ipo chini ya taasisi ya Athaql Akbaru katika mkoa wa Bagdad, kuja kushiriki katika mahafali hii pamoja na wasomaji wao wa Qur’ani tukufu.

Masikio ya wahudhuriaji yaliburudishwa na visomo vya wasomi wafuatao: Liith Abedi, msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu, Ali Jawadi Fariji, msomaji wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Bagdad na mmoja wa wasomaji wa semina ya usomaji wa Qur’ani, Mauhubu Ahmadi Mithaaq Quraishiy, mmoja wa wanafunzi wa Madrasat Aswhaabul-kisaa (a.s) na mmoja wa waliofanya vizuri katika mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, Bar’am Sajjaad Hussein kutoka katika Madrasat Aswhaabul-kisaa (a.s) na mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’ani tukufu ya Atabatu Abbasiyya inatekeleza miradi mingi ya Qur’ani, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu Tilaawah, unaolenga kunufaika na vijana wenye vipaji vya usomaji wa Qur’ani hapa Iraq na kuvionyesha katika ulimwengu wa kiislamu, sambamba na kuendeleza vipaji hivyo chini ya utaratibu rasmi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: