Miongoni mwa mafunzo ya Skaut ya Alkafeel ni (mihadhara makini)…

Maoni katika picha
Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi ya Atabatu Abbasiyya tukufu hutoa mafunzo mbalimbali kwa kufuata utaratibu uliowekwa na kamati ya wasomi na wenye masomo tofauti, wanajitahidi kutumia fursa vizuri katika kuwajenga watoto kiakili na kimwili, miongoni mwa ratiba zao, ni ratiba ya (Safari ya ufumbuzi), masomo ya ratiba hiyo yamehusu uandaaji wa muhadhara mzuri katika upande wa maandishi na uwasilishaji.

Masomo hayo yalikua ya siku tano, saa (15) za kusoma yalijikita katika vipengele vifuatavyo:

  • - Kuandaa muhadhara.
  • - Njia za kutoa muhadhara.
  • - Njia za kufanya utafiti kielimu.
  • - Njia za kuamiliana na utakacho kutana nacho.
  • - Kujenga uwezo binafsi na kuimarisha kujiamini wakati wa kuongea.
  • - Kujenga ushujaa wa maneno na namna ya kukabiliana na hadhira.

Masomo hayo yalisimamiwa na kamati ya wataalamu waliofanya kazi ya kugawa alama za washiriki chini ya kanuni maalum, tumefanikiwa kuwa na wahitimu wengi.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inaratiba nyingi za kukuza na kulea vipaji mbalimbali ndani na nje ya Ataba tukufu, ratiba nyingi zinalenga wanafunzi kwa ajili ya kuhakikisha wanapata mafundisho bora ya dini yao, kwa mujibu wa mwenondo wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s) sambamba na kuwafundisha uzalendo wa kulipenda taifa lao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: