Ufunguzi wa mradi wa kupauwa Mukhayyamu Husseiniy na kubadilisha madirisha yake

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s) na baada ya kufanya kazi kwa miaka mitatu mfululizo, Atabatu Husseiniyya tukufu imefungua mmoja wa miradi yake muhimu na mkubwa, nao ni mradi wa kupauwa Mukhayyamu Husseiniy na kubadilisha madirisha yake manne, yaliyo wekwa sehemu ya hema la Imamu Hussein, bibi Zainabu, Qassim mtoto wa Imamu Hassan na Imamu Sajjaad (a.s), na kulifanya paa liwe na muonekano mpya mzuri unaopendeza kutokana na kusanifiwa vizuri na kutiwa nakshi za kiislamu.

Hafla ya uzinduzi imefanyika katika Mukhayyamu Husseiniy, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ilipata mahudhurio makubwa ya viongozi mbalimbali na ujumbe ulio wakilisha sekta tofauti, ukiwemo ujumbe uliowakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu, ukiongozwa na katibu wake mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar (d.t).

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai (d.i) katika ujumbe aliozungumza, amesema kua: “Hakika ujenzi wa miradi ya kitamaduni, afya na malezi, unakusudia kufikia lengo kubwa ambalo ni kuwatumikia wananchi, hakika miradi hii inayofanywa na Atabatu Husseiniyya ni sehemu ya kutoa huduma kwa mazuwaru watukufu, kwa mfano mradi wa kupaua eneo hili, na mfadi wa uwanja wa haram ya Aqilat Kubra”.

Akabainisha kua: “Kuna watu wengi waliosaidia kufanikiwa kwa miradi hii katika mji mtukufu wa Karbala”. Akaishukuru wizara, taasisi za serikali na serikali ya mkoa wa Karbala kwa ushirikiano wao unaosaidia kufanikiwa kwa miradi mingi.

Katika hafla hiyo ya ufunguzi kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya tukufu amekabidhiwa funguo za madirisha mapya, na ikaonyeshwa filamu inayo onyesha upauwaji wa Mukhayyamu Husseiniy, pia zikasomwa kaswida za kishairi kuhusu tukio hilo na washairi mahiri bwana Abu Muhammad Almiyahi na Ali Swaffaar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: