Kituo cha turathi za Samara kinajadili njia za kushirikiana na kituo sawa na hicho katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Samara chini ya Atabatu Askariyya tukufu kinatafuta njia za kushirikiana na kufanya kazi pamoja na kituo kama hicho katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hayo yamesemwa katika ziara waliyo fanya ikiongozwa na mkuu wa kituo hicho Dokta Mushtaaq Asadiy katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambacho kina vituo vya turathi (Karbala – Hillah – Basra).

Ugeni huo umepokelewa na Shekh Ammaar Hilali Rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, alipokea ugeni na akasifu kazi nzuri zinazofanywa na kituo cha kuhuisha turathi za Samara, kwa kubeba ujumbe wa kuhuisha turathi, akaonyesha utayali wa kutoa msaada na kufanya kazi kwa kushirikiana kwa ajili ya kuhifadhi turathi za Ahlulbait (a.s), akasisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi na kuendelea kutembeleana kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano katika kila sekta inayo husu turathi.

Mkuu wa msafara alielezea kazi kuhimu zilizo fanywa na kituo chao tangu kianzishwe hadi sasa, akasisitiza kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa kushirikiana na vituo vya turathi vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuwatumikia Ahlulbait (a.s), akasisitiza umuhimu wa kuendelea kutembeleana ili kupata matokeo mazuri katika kuenzi turathi za kiislamu.

Mwishoni mwa ziara hiyo pande zote mbili zilipeana zawadi zilizo wakilisha mafanikio yao, ambapo kitengo cha turathi za Samara kiliipa Dar’i kituo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: