Malalo tukufu ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imefanyiwa upanuzi hivi karibuni unaofurahisha jicho la mtazamaji, ikiwa ni pamoja na kuweka vizuwizi (kuta) zinazo tenganisha sehemu ya wanawake na wanaume wakati wa kufanya ziara, pamoja na kuweka taa za kisasa na kutandika busati mpya za kifahari ambazo zimeleta muonekano mpya unao ng’arisha dirisha tukufu na kulipendezesha kutokana na nakshi nzuri zilizopo, mazulia hayo yenye rangi nzuri na nakshi za kupendeza yametandikwa katika korido za haram zinazo zunguka sehemu ya dirisha tukufu.
Kazi hii imefanyika sambamba na kufanyiwa usafi haram yote pamoja na kupigwa deki na kupulizia mafuta uzuri (manukato), miongoni mwa manukato hayo kuna yaliyochanganywa na maji ya kupigia deki na mengine yalipuliziwa angani ndani ya Ataba, pamoja na kuwekwa katika feni maalum zinazo puliza manukato, hakika ni manukato juu ya manukato ya mwenye utukufu na uaminifu Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kamera ya mtandao wa Alkafeel imeshuhudia kazi ya utandikaji wa mazulia hayo iliyofanywa usiku mwingi na inakuletea picha hizi.