Chuo kikuu cha Ummul Banina (a.s) cha kielektronik kimeanza kusajili wanafunzi wa mwaka mpya wa masomo

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha kielektronik Ummul Banina (a.s) cha kuandaa mubalighaat (wahadhiri wa kike) ambacho kipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kuanza usajili wa msimu mpya wa masomo, na kimetoa wito kwa wakinadada wanaopenda kujiunga wajitokeze katika usajili, ili waweze kuingia katika uwanja huu wa kielimu unaosaidia mwenendo wa tablighi upande wa wanawake, chuo hicho ambacho makao makuu yake yapo katika mji wa Najafu kimebainisha kua kila mwanamke anaye taka kujiunga aingie katika anuani ya usajili ifuatayo: https://goo.gl/HGYZpr na azingatie masharti yafuatayo:

  • 1- Asiwe chini ya umri wa miaka (20) na sio daidi ya miaka (45).
  • 2- Awe amemaliza masomo ya sekondari (upili) au yanayo fanana na hayo.
  • 3- Asipate chini ya alama (%60) katika mtihani wa majaribio utakaotowela katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 4- Awe na barua ya utambulisho kutoka kwa mwakilishi wa Marjaa au mmoja wa viongozi au Ustadhi anaejulikana katika chuo hiki.
  • 5- Ajaze fomu ya kujiunga katika mtandao uliotajwa hapo juu.

Kuhusu nyaraka zinazo takiwa; chuo kikuu kimefafanua kua:

  • 1- Barua ya utambulisho kutoka kwa mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu au kiongozi wa kidini au Ustadhi anaejulikana.
  • 2- Fotokopi ya kitambulisho cha makazi au cha uraia (pande zote mbili katika karatasi moja).
  • 3- Cheti cha kumaliza elimu ya sekondari (upili).

Kumbuka kua lengo la kuanzishwa chuo hiki ni kuandaa kizazi cha mubalighaati bora kwa ajili ya kufikisha sauti ya mapambano ya Imamu Hussein (a.s) kila sehemu ya dunia, na wasaidie kutoa mawaidha ya Dini yasiyokua na chuki. Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni imefungua chuo kikuu cha masomo ya hauza ya wanawake kwa njia ya masafa na kuipa jina la (Chuo kikuu cha Ummul Banina (a.s)) kwa ajili ya kuandaa mubalighaati.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: